"Sina cheo [katika
al-Shabaab] kwa wakati huu wala sijioni mwenyewe kushika cheo chochote kwa siku
zijazo," Mjahidina wa Kenya Ahmad Iman Ali alisema wakati wa mahojiano ya hivi
karibuni na Kituo cha Vijana wa Kiislamu cha Kenya. [Jalada]
Na Bosire
Boniface, Garissa
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Kituo cha
Vijana wa Kiislamu cha Kenya (MYC), Mjahidina wa Kenya Ahmad Iman Ali alikana
jukumu lake la uongozi ndani ya al-Shabaab na kutoa kauli ya kujisalimisha na
utiifu wake kamili kwa kiongozi wa juu wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane.
"[Tu] nahitaji kuelewa kwamba kutoa utiifu wetu
kwa kamanda wetu [Godane], wakati tunamsikiliza na kumtii kwa kile ambacho
hakikatazwi kunachukuliwa kama ibada ya lazima [tendo la ibada], na ninamshukuru
Allah SW [Apewe utukufu na kutukuzwa sana] kwamba ninatimiza majukumu yangu
pasipo kulazimishwa na mtu yeyote," alisema katika mahojiano yaliyoshapishwa
tarehe 4 Julai kupitia Twitter.
Hii ni mara ya kwanza Ali -- ambaye huko nyuma
alitajwa kama "Emiri mkuu wa Kenya wa al-Shabaab" -- amezungumza hadharani
kutoka alipoondoka kwenye taifa lake la uraia la Kenya kwenda Kismayu mwaka 2009
pamoja na mamia ya askari wa Kenya.
Wakaazi wa wilaya
ya Warta Nabada ya Mogadishu, ambayo ilikuwa ikijulikana kama Wardhigley,
walikamatwa wakati wa operesheni ya polisi tarehe 21 Mei kuwaondoa wanachama wa
al-Shabaab katika mji mkuu wa Somalia. [Na AFP/AU UN 1st Photo/Tobin
Jones]
Kiapo cha utiifu cha Ali kimekuja wakati Godane
akiwa anapigana na uasi wa wazi kutoka kwa idadi kadhaa ya viongozi waandamizi
wa al-Shabaab wanaompinga kwa kile wanachokiita utawala wake dhalimu.
Hata hivyo, sharti la Ali la utiifu "wa kile
kisichokatazwa" halina uzito kwa sababu maulamaa na wanazuoni wa Kiislamu
walikosoa uhalali wa tafsiri ya dini ya Godane. Matumizi ya Godane ya misemo ya
Nabii Mohammed na mistari ya Qu'ran nje ya muktadha kuhalalisha mauaji ya
wanaompinga ni kuharibu Uislamu, Kiiongozi wa dini wa Somalia aliiambia Sabahi,
kwa hiyo wafuasi wa Godane hawalazimishwi kumtii kiongozi wa al-Shabaab katika
vitendo vya dhambi.
Akiuliza iwapo jihadi inapaswa kuwa ya kidunia
au katika mawanda ya eneo -- suala lililo la kimkakati ambalo limekuwa suala
lenye utata miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab -- Ali alionekana kuwa sambamba
na Godane. "Jihad ni ya aina mbili : mashambulizi na kujilinda, na kujilinda
kunapewa kipaumbele," alisema.
Akiri uasi mkubwa, akana jukumu la uongozi
katika al-Shabaab
Ali alikiri kuongezeka kwa kiwango cha waasi,
lakini alikana tuhuma kwamba aliwaacha askari vijana wakiwa wamekwama katika
uwanja wa mapigano.
"Sijasikia yeyote aliyekimbia kwenye uwanja wa
mapambano na kutumia jina langu kama kisingizio, kama walikuwepo huko nina
wapongeza kwa unyofu wao," alisema. "[Mimi] siko katika nafasi ya kutoa
uhakikisho."
Ali alikiri kulikuwepo na idadi kadhaa ya
askari wa Kenya "ambao walidai kuondoka Somalia kwa sababu sijawasaidia
kamwe".
"Safari yangu ya kwenda kwenye jihadi ilikuwa
jukumu ambalo niliahirisha kwa muda mrefu na nilikuwa nikiwashauri vijana, kila
saa, kwamba jukumu letu liko katika uwanja wa mapambano. Kwa hivyo yeyote
anayefikiri kuwamba niliwaondoa kwa sababu ya madaraka na umaarufu, jibu langu
ni ndiyo lakini madaraka na umaarufu, [viko] akhera [baada ya maisha], siyo
katika dunia hii," alisema.
Ali aliendelea kupinga kwamba hajawahi
kuchaguliwa kuwa amiri mkuu wa al-Shabaab Kenya mwezi Januari 2012 -- ambao MYC
ilithibitisha kwa wakati huo, akiita "utambuzi kutoka kwa ndugu zetu wa Somalia
ambao wamekuwa wakipigana bila kuchoka dhidi ya wasioamini kuhusu umuhimu wa
Wajahidina wa Kenya nchini Somalia".
Hata hivyo, Ali alisema hajawahi kusikia
tangazo kama hilo. "[Kama] nilivyosema sijawa na cheo, mimi ni Mjahidina
[mpiganaji wa jihadi] kama walivyo wajahidina wengine wowote kwa hivyo
kunichukulia kama amiri nchini Kenya haina mafanikio wala kushindwa kwani nafasi
yenyewe haipo ," alisema. "Kama nilivyosema mwanzo sina cheo kwa sasa na wala
sijioni mwenyewe kuwa na cheo kwa siku zijazo."
Uchambuzi wa kufa moyo kwa al-Shabaab
Pamoja na mahojiano kutaka kuwashawishi wafuasi
kujiunga na mapigano huko Somalia, Ali bila ya kukusudia alibaini zaidi juu ya
mapigano ya nguvu na mienendo ndani ya kikundi kisichoungana na kilichokufa
moyo, alisema David Ochami, mwandishi wa habari anayeishi Mombasa ambaye
anaandikia gazeti la The Standard la Kenya kuhusu vikosi vya wanamgambo
Mashariki ya Kati na Pembe ya Afrika.
"Inaonyesha mahojiano yalipangwa na kusimamiwa
na al-Shabaab kuonyesha kwamba wapiganaji wameungana chini ya kiongozi wa
al-Shabaab Ahmed Abdi Godane," aliiambia Sabahi. "Kwa kuahidi utii kwa Godane,
al-Shabaab inatuma ujumbe huo kwa wapiganaji wanaoasi na wanaoukosoa uongozi wa
Godane kubadilisha mawazo yao na kurejea katika kundi hicho."
Alionyesha katika majibizano ya ujumbe wa moja
kwa moja kati ya MYC na al-Shabaab katika Twitter siku mbili kabla ya mahojiano
kuchapishwa kama ushahidi ambao labda ulifanyika na al- Shabaab huko Somalia na
kutumwa kwa MYC kutangazwa.
Kwa kufuta nafasi ya Ali miezi 18 baada ya
kutajwa, al-Shabaab iko wazi mno kumuonyesha Godane kama nguvu pekee ya kati,
alisema Ochami.
"Katika umma, Ali anajifanya kama kibaraka kwa
kukubali kuonekana mbaya, lakini ushushaji wa cheo ungeweza pia kufanya
kutoridhika zaidi miongoni mwa wafuasi wake ambao wanamuona kama kiongozi,"
alisema.
Kupotosha yaliyopita, kuwabughudhi raia
Katika mahojiano, Ali alijaribu kuchochea hisia
za kisasi kwa kulinganisha mapigano ya wanamgambo wa al-Shabaab wa Kenya na
majanga yasiyohusiana ya miongo iliyopita.
"Eneo la vita bado halijapitiwa kwa matangazo
ila kwa uadui unaoonyeshwa na makafiri [makafiri] hata kama hakuna anayefanya
matangazo yoyote yanayohusika," alisema. "Kwa hiyo Kenya lilikuwa ni eneo la
vita tangu wakati wa mauaji ya Wagalla."
Tukio la mwaka 1984 lilikuwa ni matokeo ya
mapigano ya muda mrefu kuhusu ardhi kati ya koo za Kiislamu za Degodia na
Ajuran. Katika tukio hilo, maofisa waliopelekwa kurejesha amri waliwaua maelfu
ya watu, ambayo serikali ya Kenya ilikiri mwaka 2000.
Katika ripoti iliyowasilishwa kwa Rais Uhuru
Kenyatta tarehe 21 May, Tume ya Haki ya Kweli na Maridhiano iliorodhesha aina za
uvunjaji wa haki za binadamu kutokana na tukio la Wagalla na matukio mengine, na
kutoa mapendekezo kuzuia kujirudia kwa historia. Ripoti itawasilishwa katika
bunge kwa ajili ya majadiliano katika tarehe ambayo bado haijapangwa.
Kurejelea mauaji ya Wagalla ni jaribio rahisi
ya kushawishi raia kwa kuchochea hisia miongoni mwa wakaazi wa Wajir wanaopenda
amani, alisema Kamishna wa Kaunti ya Wajir Naftali Mung'athia.
Hadi wakati wa mahojiano, MYC ilithibitisha
shughuli zake za kijihadi kuhusu ushiriki wa Kenya katika Misheni ya Afrika ya
Mashariki nchini Somalia na urejeshaji wa serikali ya Somalia. Hata hivyo,
katika mahojiano haya, kikundi kilirekebisha nafasi yake na kutumia migogoro ya
koo nchini Kenya kuwavutia wapiganaji wapya, alisema Mung'athia.
Mahojiano yasiyokuwa ya kawaida ya Ali pia ni
jaribio la kutengua uharibifu uliosababishwa na mwanajihadi aliyezaliwa Marekani
Abu Mansoor al-Amriki, ambaye alielezea kwa undani kuhusu kutoelewana miongoni
mwa viongozi wa al-Shabaab kuhusiana na mkakati wa kikundi, alisema.
"[Al-Amriki] alifanya uharibifu mkubwa na
kikundi kinajitokeza wakati hayupo tena katika eneo la tukio katika jaribio la
kurejesha propaganda zao katika mstari na kuokoa sura," aliiambia Sabahi.
Kumuuliza mtu kama Ali, ambaye kwa msisitizo
anakanusha kushikilia nafasi yoyote katika vyeo vya al-Shabaab, kufanya
mahojiano kunaashiria ufafanuzi wa Godane ni kwa ajili ya kuungwa mkono, alisema
Meja mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya Bashir Hajji Abdullahi.
Godane amekwishiwa na washirika katika jitihada
zake za kuwa na mamlaka kamili ya kikundi hicho kilichotengana, lakini mahojiano
haya hayataweza kuwashawishi waasi kurejea katika kikundi, alisema.
"Uharibifu ulifanyika kwa alivyofanyiwa [Abu
Mansoor al-Amriki] na viongozi wengine wa al-Shabaab," aliiambia Sabahi. "Askari
wa miguu wanaangalia usimamizi wa viongozi wao na kuhitimisha kwamba jambo hilo
hilo litatokea kwa wa vyeo vya chini."
Chanzo - abahionline.com