Paka
mwenye jina Marsik wa Urusi amesafirishwa na ndege binafsi ya Paramount
Business Jets (PBJ), kutoka Urusi hadi Marekani kwa gharama ya dola laki
moja ambazo ni sawa na shilingi milioni 162 za Tanzania.
Akisafiri kutoka Urusi hadi Marekani, Marsik anadaiwa kupata huduma ya nguvu kabla hajapanda na ndani ya ndege hiyo.
Vyeti vyake vya afya vinavyoonesha chanjo alizopata alivipata saa 24 kabla ya safari kuanza.
Tajiri
huyo anadai kutumia kiasi chote hicho ili kuhakikisha kuwa paka wake
anafika Marekani salama na kuepuka kunyanyasika ama kifo kwakuwa baadhi
ya wanyama wanaosafiri kwa ndege za kawaida huwekwa kwenye sehemu ya
mizigo hupoteza maisha.