Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh
(Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban
Ki-Moon baada ya Mkutano wa 67 wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa
(UNBoA), Jumanne, 23 Julai, 2013 mjini New York, Marekani.
Bodi
ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa saini ripoti 15
zilizoidhinishwa. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Ludovick S. L. Utouh
(Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania),Bw. Lui Jiayi
(Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China) na Bw. Amnyas
Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza).
Wajumbe
wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa katika picha ya
pamoja. Kuanzania kushoto ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania), Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi
Mkuu wa Serikali ya Uingereza) na Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China)
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh
(Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Hellen Clark Mtendaji
Mkuu wa UNDP (wapili kushoto) baada ya mazungumzo ya pamoja na
menejimenti ya shirika hilo.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa UN Women Bi. Lakshmi Puri (Kulia) wakiwa katika picha
ya pamoja na Bw. Ludovick S. L. Utouh mara baada ya kikao cha pamoja cha
kilichofanyika makao makuu ya Ofisi, mjini New York Marekani.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tuvako
Manongi (Watatu Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara baada ya kikao kazi
kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania, New York Marekani.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh
(Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi
(Katikati) na Bw. Justin Kisoka mmoja kati ya Maafisa Balozi wa Umoja wa
Mataifa, nchini Marekani.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Modest Mero
(Watatu Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alipowatembelea, UN Plaza, New York Marekani