Muimbaji wa THT Barnaba Elias amesema mama yake mzazi amefariki mapema mno na akiwa na umri mdogo.
Msanii
huyo ambaye yeye na Amini wanaunda kundi liitwalo Gemini alikuwa
akiongea na kudai kwamba wimbo wao mpya ‘Why Mimi’ una uhusiano na
msiba huo wa mama yake aliyefariki mwezi uliopita.
“Mimi
mama yangu obvious nilikuwa nampenda sana. Mama yangu ndio mtu ambaye
alisababisha Barnaba na ndio nimesimama hapa mnaniona Barnaba,”alisema na kuongeza
“Mzee
yupo lakini power nyingi niliipata kwa mama, wote walikuwa wananisaidia
vizuri lakini mama nilimzoea kwasababu mama alikuwa kipenzi changu
zaidi ya kipenzi, mshkaji wangu zaidi ya mshkaji rafiki yangu wa dhati.
"Nilikuwa
na uwezo wa kumwambia vitu vyangu vya ndani, nikamshirikisha
akanisaidia, akanipa mawazo, tukataniana, tukacheka. Kwahiyo ni vigumu,
ni neno ambalo huwa linarudi lakini siwezi kumkufuru mwenyezi Mungu.
"Ni
neno ambalo huwa najiuliza why mimi? Sababu mama yangu amefariki akiwa
kijana sana na ni ghafla sababu mama yangu mimi hakuumwa, kafa tu
pressure, kwikwi, akapoteza maisha.”