Mwanamke
mmoja mfaransa (52) amejikuta mikononi mwa polisi wa jiji la Paris
katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye chumba cha mtihani
akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19, huku
akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie.
Ripoti
kutoka nchini humo zinasema mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la
Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amevaa skin jeans na
viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae.
Lakini
jicho makini la msimamizi wa mtihani lilimnasa mama huyo kwa kuwa
msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya mtihani wa
Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake na sura
yake ya kiutu uzima.
Msemaji
wa Polisi wa Paris alisema mwanamke huyo alikiri makosa yake ya
udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza zaidi
Kiingereza zaidi ya mwanae.
Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya udanganyifu na anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000.
Lakini pia binti yake anaweza kupata msala wa kuzuiwa kufanya mtihani wowote wa kitaifa kwa muda wa miaka mitano.



