Askari
Polisi na Mgambo wa Jiji wakiimarisha ulinzi katika eneo lamanzese
jijini Dar es salaam jana, baada ya kutokea vurugu kati ya mgambo na
Wamachinga zilizosababisha barabara ya Morogoro kufungwa kwa muda kwa
saa tatu
Dar
es Salaam. Mapambano kati ya Polisi na wafanyabiashara ndogondogo,
maarufu Machinga, katika eneo la Manzese, yamesababisha kizaazaa na
kusababisha uharibifu wa mali na kufungwa barabara, kusimamisha shughuli
zote kwa zaidi ya saa tatu.
Hali
hiyo ilitokea baada ya ‘Wamachinga’ ambao waliondolewa kwenye maeneo
yasiyoruhusiwa kwa biashara wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa
Marekani nchini, kuamua kurejea kwa nguvu katika maeneo hayo.
Shughuli
za kijamii na kibiashara katika eneo la Manzese, zilisimama kwa
takriban saa tatu kutokana na eneo hilo kugeuka uwanja wa vita na
usalama wa wananchi wasiokuwa na hatia kuwa shakani.
Awali
polisi walitoa tangazo la kuwataka Machinga hao kuondoka katika eneo
hilo agizo ambalo halikuwe za kukubaliwa, jambo lililosababisha kutumika
kwa mabomu ya kutoa machozi.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Tukio
hilo la Polisi kutumia mabomu hayo lilianza saa 7 mchana hadi saa 9.45,
waliposimamisha kutumia mabomu ambayo yalikuwa yakifyatuliwa
kuwatawanya Machinga hao.
Wakati
Polisi wakizunguka kuwatawanya, machinga nao walikuwa wakiweka mawe na
magurudumu ya magari barabarani kuhakikisha magari ya askari hao
hayapati nafasi ya kupita.
Mitaa
ya kuzunguka eneo hilo ambalo mara nyingi huwa na mkusanyiko wa watu,
lilionekana kuwa wazi huku Polisi wakilitawala kwa kuzunguka huku na
kule kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Mwananchi
Jumapili lilishuhudia gari la polisi aina ya Land Rover likiwa limejaa
wafanyabiashara hao waliokamatwa wakati wa kuwaondoa eneo hilo, ambalo
ni kandokando ya barabara inayojengwa ya mabasi yaendayo kasi ya
Strabag.
Baadhi ya wafanyabiashara wenye maduka, walijifungia ndani ya maduka yao kuepuka wizi ambao ungeweza kutokea.
Taarifa
zinaeleza kuwa baadhi ya mali ambazo zimeharibiwa katima vurugu hizo
pamoja na kuchomwa moto kwa jengo la tawi la Klabu ya Yanga eneo la
Manzese.
Baada
ya barabara kufungwa kwa mawe na wamachinga hao, hali hiyo ilisababisha
foleni na usumbufu kwa wenye magari, waliokuwa wakitoka Ubungo kwenda
Karikaoo na wale waliokuwa wakitoka Karikoo kwenda Ubungo iliwabidi
kutumia njia za vichochoro kuepuka vurugu hizo.
Wakati
polisi wakifyatua mabomu hayo, baadhi ya watu walikuwa wakikimbia ovyo
huku watoto wakilia bila ya kupata msaada wa kuwaondoa katika eneo hilo.
Baadhi
ya watu walilazimika kupanda juu ya Daraja la Manzese ili kukimbia
mabomu ya Polisi yaliyokuwa yakilipuliwa mfululizo kuwatawanya
wafanyabiashara hao.
Askari
hao walifyatua mabomu hayo katika mikusanyiko yoyote, bila ya kujali
hata wale waliokuwa katika sehemu za baa na migahawa wakipata vinywaji
na chakula.
Mfanyabiashara
Steven Frank akizungumzia tukio hilo alisema, Polisi wametumia nguvu za
ziada kuwatawanya kitendo ambacho kama wangetumia njia ya kistaarabu
wangeweza kutekeleza agizo hilo.
“Palikuwa
hakuna sababu ya kufyatua mabomu yao ovyo, kwani sisi hatukuwa
tunawapiga wala nini lakini wao wanafyatua tu bila mpango,” alisema
Frank.
Mwananchi
Jumapili alimsikia mmoja wa Polisi hao akiwasilia na mwenzake kuwa kama
wamemaliza mabomu kuna mengine yapo ndani ya gari.
“Kuna
katoni kama tatu hivi katika gari, hivyo kama mtamaliza tutawasiliana
ili tuweze kuwaongezea, lakini inatubidi tufyatue tu kuwatawanya huku
tukiimarisha ulinzi na usalama wa wananchi,” alisikika Polisi aliyekuwa
amevaa kiraia.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipotafutwa
kuzungumzia suala hilo alisema hana taarifa zozote.
Alimtaja
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura kwamba ndiye
anayeweza kuzungumzia suala hilo. Hata hivyo Wambura alipotafutwa
hakuweza kupatikana.
Mmoja
wa wafanyabiashara wa eneo hilo, Bashir Zacharia alisema tukio hilo
limewasikitisha kwani hawana sehemu ya kwenda ambayo watafanya biashara
kwa wingi.
MWANANCHI