Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Wednesday, July 3, 2013

KANYE WEST AKATAA KUUZA PICHA YA MWANAE KWA MAMILIONI YA PESA

Watu wengi walitegemea kuiona picha ya kwanza ya mtoto North West hapo jana lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo. Haitaweza kutokea. Ripoti ya karibuni inafichua kuwa Kanye West na Kim Kardashian wamekataa ofa za mamilioni ya dola za kimarekani zilizotoka kila pande kwaajili ya kuuza picha ya mtoto wao.

Wenyewe Kanye na Kim wanasema mtoto wao hauziki kwa pesa yoyote ile.

Tangu Kim alipojifungua mapema kuliko ilivyotarajiwa Juni 15, ofa kubwa iliyotolewa kwa wazazi hao wenye kujiskia ilitoka kwa jarida moja la Australia wakiwa wameweka mezani dola milioni 3. Lakini kiasi hicho hakikutosha na hakuna kiasi kitakachotosha.

Ripoti za awali zilisema kwamba kama wazazi hao waataamua kuuza picha ya kwanza ya mtoto wao, basi pesa zote zitakwenda kusaidia mambo ya kijamii.

Lakini mpaka muda huu inaonekana kama vile na wao wameamua kufuata nyayo za Beyoncé na Jay-Z, ambao walizuia picha za mtoto wao Blue Ivy Carter kwa karibu mwaka mzima.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...