Kamati ya kuchunguza bei ya vyakula katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyoudwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Rehema Chimbi imebaini kuwa hadi sasa bei ya vyakula haijapanda katika masoko na maeneo mbalimbali mkoani Dodoma.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo Alhaji Mussa Kasmir amesema hayo leo wakati akiongea na
waandishi wa habari kwenye ukumbi uliopo kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa
Dodoma.
Alhaji
Kasmiri amesema kuwa kamati hiyo iliyoundwa kuchunguza bei
imemshirikisha afisa biashara mkoa ,Mwenyekiti wa TCCIA mkoa na afisa
masoko na.
Amesema kuwa walitembelea masoko yote na kubaini kuwa hakuna badiliko la bei.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa kamati imefanya uchunguzi katika maghala ya chakula na amewahamasisha wafanya biashara kutopandisha bei katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani na atakayekiuka atachukuliwa hatua stahiki.
CHANZO: Redio Mwangaza FM, Dodoma-Tanzania