Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepokea taarifa kwamba
waandishi wa Habari kadhaa wamepelekwa Mtwara kwenda kumhoji msichana
mmoja kwa madai ya kubakwa na wananjeshi wa JWTZ.
JWTZ linapenda
kuwafahamisha wananchi kuwa endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye
baadhi ya vyombo vya Habari wazipuuze kwani hazina ukweli wowote
zaidi ya kuwa ni za upotoshaji.
Msichana
huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba
maafisa na askari wa JWTZ waliopo huko Mtwara wanafanya kazi kwa
uangalizi wa karibu na vitendo hivyo vya aibu hawawezi kuvifanya.
Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.
Tunapenda kuwafahamisha watanzania wote kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
Tunasikitika sana kama wapo watanzania wenye mawazo hayo machafu
ya kulichafua JWTZ lenye sifa nyingi ndani na nje ya nchi yetu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 92023, Simu: 0764 742161