Kuna
saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz
watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko
skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza
kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa
kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better”
alifunguka Uwoya.
Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.
Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.
Kama hukufanikiwa kusoma habari hiyo iliyoripotiwa na Globalpublishers basi isome hapa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
SIRI
nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa
wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
KISA KAMILI
Huku
akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu,
kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka
kwa muda kwa Uwoya.
Kwa
mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond
kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha
Uwoya kutoa maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya
kumchukia kila walipokutana. NA GPL
UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua
Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi
alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia
mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo
zilichochea.
“Kufuatia
hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na mashosti wa
Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya Warembo’
alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya ampende.
CHIKOKA ATAJWA
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka.
“Chikoka
hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma sana lakini siku
moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka, maeneo ya Sinza-Mori
(Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo ndipo uhusiano
ulipoanzia.
“Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya.
GLOBAL NOMA
“Diamond aliomba ahadi ya
kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya aliiva na kukubali
ambapo walikutana kwenye ile hoteli mliyoandika (Global) kule Mbezi
Beach (Dar) wakamalizana.
“Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya.
“Kwa hiyo utagundua chanzo
cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda Diamond kwani alikuwa
akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,” kilidai chanzo chetu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya kujazwa habari
hizo, mwanahabari wetu alilazimika kumtafuta Diamond ili kuhakikisha
kama alichoelezwa kina ukweli ndani yake ambapo bila kinyongo, mkali
huyo wa wimbo wa Kesho alifunguka:
“Dah! Japo yalishapita ila ni kweli Uwoya nilikuwaga nikipata taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa alikuwa ananichukia sana.
“Nilikuwa nikijiuliza
sababu za yeye kunichukia lakini nikawa sizipati hata kidogo na hata
nilipochunguza niligundua kweli alikuwa hanipendi kabisa.
“Sipendi sana kuzungumzia
ishu hiyo ila naweza kukubali kweli kuwa marafiki zake na wangu ndiyo
walionichochea sana kukutana na Uwoya na sasa hatuna tatizo na tunaishi
kwa amani na upendo ingawa mengi yamepita na yaliyosemwa sina sababu ya
kuyashikilia, kikubwa tumuombe Mungu.”
KAMA KAWA UWOYA HAPOKEI SIMU
Ili kupata mzani wa habari
hiyo, gazeti hili lilimwendea hewani Uwoya lakini kama kawaida, simu
yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita,
gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari ya Uwoya na
Diamond kunaswa usiku katika moja ya vyumba vya hoteli maarufu kwenye
Ufukwe wa Bahari ya Hindi huko Mbezi Beach, Dar ambapo habari hiyo
iliibua maneno lakini sasa mwanamuziki huyo amemaliza utata kwani nguzo
na sifa kuu ya Global Publishers ni kuandika ukweli siku zote.