Waasi wa M23 wa DR Congo, wanadai kuwa wamemkamata askari wa Tanzania
anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa
Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka
1994.
Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Kwa mujibu wa chimpreports.com,
M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47
yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook
ikiambatana na picha hiyo:
“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu
pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri,
walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma
tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe.
Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga
muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka
hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la
Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari
ya tanzania ambaye tulikamata”