Kijiji hiki kinapatikana katika jimbo la Overijssel, huko nchini
Uholanzi. Kijiji hiki hakina barabara na watu wake husafiri kwa
kupitia mifereji yake maridadi au kutembea kwa miguu juu ya
madaraja ya mbao yaliyopo juu ya mifereji hiyo ya maji. Kijiji
hiki kimekuwa ni kivutio kikubwa cha utalii katika jimbo la
Overijssel.