Safari
yangu kuelekea mkoani tabora ilikuwa na changamoto nyingi, Ila kubwa
namshukuru Mungu nilifika salama na kurudi salama. Najua kuna FANS wangu
wengi wananipa support haswa katika maombi ya familia yangu. So najua
itakuwa vizuri kama nitashare na nyie jinsi safari yangu nzima
ilivyokuwa.
Nimetumia siku tano so nitakuwa naielezea kwa day after day ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka naenda mpaka narudi.
Ila
wakati naipanga hii safari ili kwenda kumuona mume wangu, iliniweka
katika wakati na maamuzi magumu sana kama fans zangu mnavyofahamu nina
watoto wadogo akiwepo mdogo wa miezi mine 4, Tabora ni mbali sana ni
mwendo wa karibia masaa 14 kutokea Dar Es Salaam watoto ni wadogo
nikisafiri nao nikaona nitakuwa nawatesa, Nikafanya maamuzi magumu mno
ya kuwaacha wanangu kwa wadada wasaidizi wangu wa nyumbani. Hizi ni
changamoto za maisha inapofika wakati mgumu kama huu ulionifikia mimi
inabidi ufanye maamuzi mazito, so nikawaacha wanagu Lincon na Linstone.
Lincon na Mdogo Wake Linston.
DAY1. IJUMAA 28/06/2013
Siku
ya Ijumaa tarehe 28/June Tulikutana Ubungo, Tukitumia usafiri binafsi
na tulikuwa watu 5. Tukaanza safari yetu na tunamshukuru mungu tulifika
salama Mkoani Morogoro, Tukaendelea na safari Ila tukiwa kati ya
Morogoro na Dodoma gari yetu kidogo ikaleta tabu,
hapa ni kati ya Moro na Dom
Baridi ya hapa ilikuwa ni balaa.
hapa baba mkwe akicheki tatizo la gari.
Endelea kufuatilia tukio ili kwa kubofya hapa chini
Baada ya dk kadhaa gari ikawa iko poa.
Baada ya gari kuwa poa tukaendelea kwa safari tukaingia Dodoma, Tukapata chai kidogo
Tukisubiria Chai hapa ni Dodoma.
Baada ya chai tukirudi garini kuendelea na safari.
Na gari nayo ikapata lishe/mafuta.
then tukaendelea na safari.
Tulipofika
Ikungi Kabla hatujafika Singida mjini gari ikaharibika tena , dereva
akasema ni tatizo dogo linarekebishika fasta then tutaendelea na safari.
Tukapata Fundi pale pale Ikungi, hapa akitazama tatizo.
dah
ikawa vise versa tatizo likawa kubwa, it was around saa tisa hivi
alasiri tupo Ikungi, mpaka saa 6 usiku gari haikufaa ikabidi tutafute
hotel kulala hapo.
Mida ya saa sita hivi gari ikawa bado haijatengamaa.
DAY2.JUMAMOSI 29/06/2013
Siku
ya pili tukaamka na kujiandaa, ila mpaka tunamalizia kujiandaa gari
ilikuwa bado haijatengamaa, ili wote tusiwe tumestuck sehemu moja
tukaamua kugawana wengine wabaki na gari na wengine tutangulie. Kutokea
hapo Ikungi tukapata usafiri wa NOAH mpaka Singida Mjini si Mbali sana
ilikuwa mwendo kama wa dk 20 ama 30 hivi, Tulipofika Singida Mjini
tukapata HIACE ambayo tulianza safari kuelekea Igunga.
hapa ilibidi tufanye safari za kuunga unga mana usafiri pia ulikuwa wa tabu,
mwendo wa masaa kama mawili na nusu ama matatu tukawa tumefika Igunga, tukakata tiketi za kuelekea Tabora mjini..
Hapa ni stendi Igunga tukisubiria basi.
Usafiri ni wa Tabu mno tukapata basi ila tulikosa siti takasimama ,
it
was a very rough road kutokea hapo Igunga mpaka Tabora mjini na ni
mwendo karibu wa masaa 3 na nusu hivi, Ila Mungu alisadia tukafika
salama Tabora mjini mida ya saa 11 kama na dk 20
Mwenyeji wetu akitusaidia kutuonyesha hoteli.
Kutoka stendi ya mabasi mpaka ilipo hoteli ni mwendo wa dk 2 tu kwa miguu.
na
kuanza tafuta hotel. By the way nilitamani sana nikiingia Tabora
nielekee Gerezani Ila nilikuwa nilishachelewa kwa uliza uliza niliambiwa
Kutembelea gerezani mwisho ni saa 9 alasiri.
Uchovu wa safari.
Katika
kuulizia ulizia hoteli tukapelekwa Hotel inaitwa Mwafrika Hotel, Pale
Tulikosa nafasi ila meneja wa pale akachukua jukumu la kututafutia
sehemu nyingine , tukapata sehemu nyingine lakini tukapanga next day
wakitoka watu tutarudi pale.
Aliyevaa Jezi ni Meneja Wa Mwafrika Hoteli, Anayenielekeza ni Mmiliki wa Mwafrika Hotel.
Huyu
ni shemeji yangu kabisa kabisa, ni mume wa dada yangu"post ya
changamoto na Opportunity" mtamfahamu vyema. Hapa ndo alituchukua na
kutupeleka hotel nyingine kwa usiku huu.
DAY3. JUMAPILI
Tuliamka
asubuhi tukajiandaa kuelekea gereza Kuu Uyui, ila tulipitia Mwafrika
hotel kuacha mizigo yetu mana kwa siku hiyo tutakuwa pale.
Then safari ya kuelekea Gereza Kuu la Uyui,
Si
mabali kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5 hivi kwa Gari,
tukawa tumefika gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata
kujiandikisha na kila kitu halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana
pia tulikuta watu wengine ambao nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa
na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na sie tukaitwa katika listi
tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria zao za kuzima simu
na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko kijichumba
kidogo tu.
Kiukweli
it was a very SAD moment, nilipomuana mume wangu, akiwa kwa upande wa
pili na sikuwa namuona vizuri mana hiyo nyavu iliyotenganisha hapo
ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa Kujizui MACHOZI yalianza kunitoka, Ila mume
wangu alikuwa MORE THAN STRONG akinisihi nisilie ye yuko poa, Kiukweli
Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na mie Napata nguvu. Swali la
Kwanza aliniuliza Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako
salama , Kutokana na umbali wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia
Naendelea Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko Upande Wetu, Misukosuko
niliyoipata njiani nawaza ningekuwa na watoto ingekuwaje”?? .Tukaongea
mawili matatu kama dakika tano hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa
kutoka. Kuna nguo nilibeba tukaambiwa zikakaguliwe kwanza then ndo
atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka then tukaondoka.
Kiukweli
after kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia
kuwa yuko mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache
sana na nilikuwa na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale
wakatuambia kwa waliotoka mbali huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at
least hata dk kumi, so nikipanga kurudi tena siku ya Jumatatu.
Jioni
Baada ya Kutoka Gerezani, Nilikutana na Sister Wangu ambaye hatujaonana
zaidi ya miaka 20. Kwenye post ya changamoto na opportunity nae
mtamfahamu.
DAY4.JUMATATU
Niliamka
asubuhi na kujiandaa, Baada ya kumaliza nikatoka kwenda kutafuta baadhi
ya vitu alivyoniagiza, So nilipokamilisha vyote nikaanza safari ya
kwenda Gereza Kuu Uyui kwa siku nyingine tena, Leo nikiwa nimeongozana
na mwanasheria ambaye yeye anafanya shughuli zake kule kule kwa ajili
ya mambo mawili matatu.
Tukafuata
taratibu zao kama kawaida kuandikisha, na baada ya muda tukapata
nafasi ya kwenda kumuona, Leo Kidogo ikawa nafuu kwa vile tunatoka
mbali” ipo sheria kabisa kwa mtu mfano anayetoka mbali na Tabora kuwepa
nafasi kidogo zaidi mana ametokea mbali “. Kama Kawaida ya pale
tukatakiwa kuacha kila kitu na siimu kuzizima, tulichoruhusiwa kupita
nacho leo hii ilikuwa ni pesa tu,
Nikiwa na mwanasheria.
Tukapelekwa
katika chumba cha wazi ni pa kuonea wafunga tulikuwa chini ya ulinzi
mkali wa uangalizi wa askari si chini ya 7, akiwepo askari mmoja wa kike
, na masharti makubwa mawili hakuna kulia na hakuna kuongea kwa
kunong’ona “WHISPER”. Dah kweli ilikuwa ni wakati mgumu hali ambayo
nilikuwa naisikia uchungu then napewa masharti hakuna kulia, Ila narudia
kusema Mungu hawezi Kuniacha , Nilipata Ujasiri wa ajabu na kuacha
kulia na kuanza kuongea mawili matatu kuhusu familia na kuhusu maswala
ya kazi, Ila pia napo kama after dakika kumi tukaambiwa muda umekwisha
tunatakiwa kutoka . Tukatoka na kurudi zetu hotelini. Usafiri wa Tabora
kwa sasa ni tabu tukakosa usafiri wa kurudi Dar kwa siku ya Jumanne.
Hapa Nikiagana na Mwanasheria.
DAY5.JUMANNE
Baada
ya kukosa usafiri wa kurudi Dar Siku ya Jumanne, nikitazama Tabora ni
mbali nikasema ngoja niende Gerezani kuomba hata dakika moja ya kumuaga
mume wangu, nikaelekea gerezani Uyui, Ila dah nikaomba sana
wanilikatalia, nikaamua kurudi zangu kiunyonge hotelini, kuja kusubiria
Jumatano kusafiri kurudi zangu Dar.
DAY6.JUMATANO
Nikaanza
safari ya kurudi dar, Tuliondoka Tabora saa 12 asubuhi, After Masaa
Mengi njiani by saa 2 na nusu hivi nikafika salama Dar, nilikuwa So
excited kuwaona wanangu, Thanx God Nilifika salama na niliwakuta wanangu
wako salama.
NYONGEZA
Jumatatu
tarehe 8/Julai/2013, mume wangu anapandishwa tena mahakamani huko
Tabora, Bado nahitaji msaada wenu katika kunisaidia maombi.
SHUKRANI.
Napenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote wote ambao mpaka sasa mko pamoja
na familia yangu, Kiukweli ni wengi mno sitaweza kuwataja wote na naomba
msinihukumu kwa hilo ni wengi mno, Ila kwanza kabisa naendelea
kumshukuru Mungu naamini yuko pamoja na familia yangu, naamini
hatatuacha , pili kwa wasaidizi wangu wa kazi nyumbani kwangu
niliwaachia wanangu mikononi mwao na nikawakuta wako salama, Ndugu wote
wanaonisupport, marafiki wote wanaonisupport, Ila Shukrani zangu za
dhati pia ziwaendee FANS wangu woteeeeee popote walipo kwa kunisaidia
kwenu katika maombi inatia moyo.
Source: Joyce Kiria
Source: Joyce Kiria