Bunge
limepitisha sheria ya fedha inayoanzisha kodi kwenye Kadi ya simu. Kila
mwenye Kadi ya simu, bila kujali matumizi yake ya simu, atakuwa analipa
tshs 1000 kwa mwezi.
Kodi hii imeanza tarehe 1 Julai 2013.
Pendekezo
hili la kodi lilitolewa na waziri wa Fedha wakati anasoma hotuba yake
ya Bajeti. Lakini kwa mshtuko mkubwa nimejua leo kuwa kodi hii
iliingizwa kwenye finance bill na kupitishwa.
Kwa
kodi hii maana yake ni kwamba mwananchi wa kawaida, tuseme mwananchi
anayefanya kazi ya kuuza maandazi barabarani kila siku, analipa kwa
mwezi tshs 1000 sawa sawa na Mbunge ambaye analipwa tshs 11.2m kwa mwezi
kama mshahara bila posho za kukaa, posho ya kujikimu na safari
mbalimbali. Mwananchi muuza karanga, atalipa sawa na Bakhresa!
Kinachonishangaza
ni kwamba kuna ukimya mkubwa sana kuhusu kodi hii mpya (labda ziara ya
Obama). Kodi hii ni mbaya sana. Very rudimentary. Ingawa wabunge
wameipitisha, ni vema wananchi wasimame kukataa.