Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, July 11, 2013

HII HAPA MIKAKATI YA SIRI YA CHADEMA KWENYE CHAGUZI ZA UDIWANI HUKO ARUSHA




Mgombea Udiwani katika Kata ya Elerai kwa tiketi ya CHADEMA, Jeremiah Mpinga akielezea namna Mwigulu Nchemba, CCM, alivyofika nyumbani kwake na kumtaka aachane na siasa za CHADEMA.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Julai 14, 2013, kitahakikisha kitatumia gharama yoyote kuzilinda kura katika Kata nne jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho Mkoa, maarufu kwa jina la “Ngome”, Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alisema kuwa uchaguzi wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Jumapili katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai utakuwa wa aina yake.

Mhe. Lema alisema kinyang’anyiro hicho cha Kiti cha udiwani kitasimamiwa na vikosi maalum vya chama hicho sanjari na vijana wao wa “Red Brigade” huku Wabunge zaidi ya 16 wakitarajiwa kuwasili Arusha kwa ajili ya

kuhakikisha ulinzi wa kura unaimarika.

“Ulinzi wa kura zetu umeimarika kwa asilimia kubwa na tutashinda Kata zote kwani hadi sasa tunazo asilimia 80% ya ushindi,”alisema Lema.

Naye Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha, Joshua Nassari amelalamikia kitendo cha jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi katika mapokezi yake huku wakigomea kufanyika kwa mkutano wa hadhara jimboni kwake kwa madai kuwa utavuruga uchaguzi.

Mhe. Nassari aliyasema hayo muda mchache mara baada ya kuwasili Mkoani Arusha ambapo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili huku akiweka wazi kuwa anaendelea vizuri na yupo gado kwa mapambano

“Nimefika airpot Dar hali ni tete baada ya kuona polisi kila kona, hapa Arusha hivyo hivyo huku wakiwa na magari zaidi ya 6… Kwa nini wasilinde rasilimali za nchi? Kama tembo wanaoibiwa kila siku waje wahangaike na mimi ambaye naenda kuongea na wananchi wangu,” alihoji Nassari.

Naye mgombea udiwani wa Kata ya Elerai, Mhandisi Jeremia Mpinga amekanusha vikali tuhuma za kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha udiwani wa Kata yake kama ilivyotangazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Mpinga likwenda mbali kwa kusema kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba alifika nyumbani kwake na kumtaka aache kugombea kwa tiketi ya CHADEMA na kumwahaidi kuwa atapewa Ukuu wa Wilaya na Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

“Alinipigia Jun1 12 majira ya saa tatu asubuhi akitaka kuja kwangu kuniona, akaja, na ndipo aliponipa ujumbe huo wa ukuu wa Wilaya,” alisema Mpinga.


picha, maelezo via Jamii Blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...