Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba Emanuel Mwasibata akiwa amesimamia kikao cha usuruhishi
Dereva wa daladala Aswile Mwalukoba aliyeshika fimbo baada ya kurejea
nyumbani na kuhudhuria kikao cha usuruishi ambapo alikili kuzaa na
mwanafunzi huyo na kukubali kuzika .
Daladala iliyobeba mwili wa Marehemu kutoka Uyole.
Wakazi wa Uyole wakiwa wameshikwa na butwaa baada yakumkosa mwenyeji wao
Mwili wa mtoto ukiwa umefunkwa na kitenge na kutelekezwa kwenye kiti
Kulia ni Carolina Kyando akiwa na dada yake baada ya kuleta mwili wa
mtoto nyumbani kwa Mwalukoba eneo la Mama John jijini Mbeya
Majirani pande zote mbili wakingojea kujua hatma ya mazungumzo yanayo endelea baada ya Mwalukoba kurejea
Vitendo
vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake jijini mbeya vimeendelea
chukua sura mpya baada ya dereva wa daladala jijini humo kumzalisha
mwanafunzi Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo Ilomba.
.
Tukio
hilo limetokea hivi karibuni eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya
Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile
Mwalukoba (45 ) kutelekezewa wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada
ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumzia
tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa
mgogoro huo umetokana na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwakile
alicho dai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa
upande wake binti huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai
kuwa kitendo cha yeye kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake
unatokana kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa marakwa mara na
kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume
huyo.
Mwanamke
huyo amefafanua kuwa mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa
matibabu katika Hospital ya Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu
mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa taarifa za msiba huo.
Amesema
mara baada ya kutoa taarifa hiyo mwanaume huyo alikubali na kumueleza
mwanamke huyo kuwa yuko tayari kwa ajili ya mazikoya mtoto huyo ambapo
anafanya taratibu za kuwasiliana na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani
Rungwe.
Amesema
katika siku iliyofuata mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani
na wala hakuwepo nyumbani kwake anapo ishi eneo la Mama John hali iliyo
plelekea baadhi ya majirani na mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na
kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa lengo la kufanya taratibu
nyingine .
Aidha
majirani hao waliamua kuchukua mwili huo hadi nyumbani kwa Mwalukoba
ambapo waliuweka kwenye kiti ndani ya nyumba yake huku wakiendelea
kumsubiri mwalukoba arudi aliko ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo
akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba
hadi nyumbani hapo.
Kitendo
hicho cha kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo
Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji juu ya kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa
muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.
Baada
ya kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo
alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi
ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12
jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine
kutoka Uyole na Mama John.