Waraka
huo wa CCM uliosainiwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Jitu
Vrajilal Soni una lengo la kupinga mapendekezo mbalimbali yaliyomo
katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyozinduliwa Juni 3 mwaka
huu.
Makamu
Mwenyekiti wa Kanda ya Mashariki na Pwani, Mabere Marando akihutubia
mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja cha Shule ya Msingi
Ukombozi, Manzese jijini jana alidai waraka huo una lengo la kuvuruga
mchakato wa kupata Katiba Mpya yenye manufaa kwa Watanzania wote.
Marando
akisoma baadhi ya mapendekezo ya CCM yaliyomo katika waraka huo kwenda
kwa Jaji Warioba kumtaka kuviondoa vipengele vilivyomo ndani ya Rasimu
ya Mabadiliko ya Katiba Mpya vinavyohusu Tunu ya Taifa, kuwa bila
kufanya hivyo hakutakuwa na tija ya uwajibikaji.
Alizitaja
tunu hizo za taifa kuwa ni kuwa utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi,
uwajibikaji na lugha ya Taifa ambazo Chadema wanaziunga mkono zipite na
kuwa sheria.
“Sisi
Chadema tunaona zinafaa kutokana na umuhimu wake lakini CCM wamemwambia
Warioba aondoe neno uwazi wakiwa na maana ya kuwa wanataka mambo yao
yasiwekwe wazi,” alisema Marando.
Marando
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema, Jaji Warioba
amependekeza utajiri wa taifa uendelezwe na kuzuia mtu kumnyonya
mwenzake jambo ambalo CCM wamelipinga.
“CCM
katika waraka huo ibara ya 11.2 na 11.3 wamemwambia Warioba viondolewe,
sasa viongozi wa CCM na Chadema ni kina nani wanawapenda wananchi
wake,” aliwauliza wananchi waliojitokeza katika mkutano huo na kujibiwa
na kelele kuwa ni Chadema.
Marando
alisema katika kipengele cha maadili ya taifa na jamii kinachosema
viongozi wanatakiwa kuzingatia uongozi, utoaji wa huduma, kufanya usawa
na kupiga vita rushwa mapendekezo ambayo yakipita kuwa sheria yatasaidia
kupunguza tatizo la rushwa la utoaji wa huduma uliotukuta.
“CCM
ambao hawaonyeshi dhamira ya kumkomboa mwananchi wake, wamemwambia
Warioba kuyaondoa maadili hayo kwani hayafai, sasa kupiga watu, kula
rushwa kweli liondolewe? Hawa CCM kweli hawataki tupate katiba ya
kuwakomboa wananchi,” alisema Marando na kuongeza:
“Kama
hiyo haitoshi wamesema kitendo cha wananchi kumwajibisha mbunge wao
kama hatakuwa anatimiza majukumu yake nao wamesema mapendekezo hayo
hayafai. Kweli CCM hawataki tupate Katiba Mpya.”
MWANANCHI
MWANANCHI