Genge
moja nchini India limekata mkono wa binti mmoja mwenye miaka minane kwa
kutumia fyekeo huku familia yake ikijaribu kuhakikisha kuachiwa kwa
kaka yake aliyetekwa nyara.
Uzma Ara alisafiri kwenda Patna, mjini Bihar, mashariki mwa India,
akiwa na familia yake kwa lengo la kumkomboa mtoto huyo wa kiume mwenye
miaka minne ambaye alikuwa amenyakuliwa kwenye mtaa mmoja karibu na
nyumbani kwao katika wikaya ya Darbhanga.
Baba wa Uzma, Ainul Ansari anadai genge hilo lilimlenga binti huyo
kutokana na kuwa shuhuda mkuu wa tukio hilo la utekwaji wa mtoto wake,
Julfikar.
Vyombo vya habari vya India vimeripoti binti huyo yuko mahututi
kwenye hospitali moja ya serikali mjini Patna baada ya kupoteza sehemu
ya mkono wake wa kulia.
Familia hiyo imesema binti huyo alishambuliwa karibu na stesheni ya treni mjini humo Ijumaa wakati wakitafuta hoteli ya kukaa.
Ansari alisema kundi hilo liliwafuata hadi Patna ambako walikuwa wanatarajia kufungua mashitaka polisi.
Serikali ya Janata Dal inayoongozwa na Waziri Mkuu Nitish Kumar sasa
imeamuru uchunguzi mpya wa shambulio hilo na mtoto wao wa kiume
aliyepotea.
Mama wa Uzma, Nasreem Khatoon alimpinga moja kwa moja waziri mkuu huyo kwenye mkutano wake wa kila wiki.
Familia hiyo inasema polisi wa eneo hilo wameendelea kumshikilia mtoto huyo aliyepoteza mkono wake kwenye ajali ya treni.
Ansari ambaye ni fundi cherehani, alisema amekuwa akilazimishwa
kulilipa genge hilo Pauni za Uingereza 3,300 kwa miezi michache
iliyopita, imeripotiwa.
Anasema kwamba polisi wamegoma kuchunguza pale familia hiyo ilipogoma kulipia zaidi, genge hilo lililomteka mtoto wao.
Wanasiasa wa upinzani sasa wameishutumu serikali ya mjini humo kwa kushindwa kuchunguza madai hayo moja kwa moja.
Msemaji wa chama cha Bharatiya Janata, Shahnawaz Hussain alinukuliwa
na Shirika la habari la Gulf akisema kwamba waziri mkuu huyo amechangia
'kuanguka kabisa kwa sheria' mjini Bihar.



