Ppe Guardiola ametangaza kumtaka Thiago ndani ya Bayern Munich
Huku tetesi nyingi za vyombo vya habari zikidai kuwa dili la usajili wa
nyota wa timu ya taifa ya Hispania chini ya Miaka 21 kwenda Manchester
United limekamilika Bayern Munich wamejitokeza na kutangaza wazi nia ya
kumsajili nyota huyo hali inayofanya kuwepo kwa vita kali baina ya
Wajerumani (Munich) na Waingereza (Man United) kuwania sahihi ya nyota
huyo (Thiago Alcantarra) .
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akizungumza na waandishi wa habari
hii leo amesema kuwa anamfahamu vizuri Thiago na angependa kumsajili kwa
kuwa ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya nne au tano .
Guardiola amesema kuwa kwa sasa mchezaji ambaye angependa kumsajili ni
Thiago na kama hataweza kushawishi kujiunga na Bayern basi hatasajili
mchezaji mwingine . Kauli hii ya Guardiola inamaanisha kuwa timu hizo
mbili za United na Bayern kwa sasa zitakuwa zikihaha kila moja ikijaribu
kumshawishi nyota huyo kusaini kwenye timu mojawapo.
Thaigo ndio ataamua kwenda United au Bayern Munich
United kwa muda mrefu wamekuwa wkaitajwa kuwa mbioni kumtangaza mchezaji
huyo kama mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kusajiliwa na David
Moyes baada ya usajili wa beki wa Uruguay Guillermo Varella na kiungo
huyo (Thiago) amekuwa akijaribu kuondoka Barcelona ambako ameshindwa
kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza .
Thiago Alcantarra ana malengo ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha
timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini
Brazil mwakani na amekuwa akipambana kuondoka Barcelona ili aende mahali
ambako atamshawishi kocha Vicente Del Bosque kumpa nafasi . Mkataba wa
Alcantara unaonyesha kuwa asipocheza kwenye asilimia 60% ya mechi za
timu hiyo anaweza kuuzwa kwa bei ya Euro Milioni 18 na kwa msimu
uliopita hakucheza kwa kiwango hicho hali inayofanya kuondoka kwake kuwa
rahisi .
David Moyes ataipata saini ya Thiago au United watapigwa bao na Bayern Munich