Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe Ezden
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, baadhi ya mastaa walioomba hifadhi ya majina yao
ambao walihudhuria ndoa hiyo iliyofungwa wiki iliyopita Ubungo jijini
Dar walisema, wamechoka na mialiko ya ndoa zake kila baada ya kipindi kifupi hivyo ni wakati sasa wa kutulia.
“Asifanye
ndoa kama fasheni, tumechoka kuhudhuria sherehe za ndoa yake, kama ana
kasoro, ajirekebishe ili atulie sasa ajenge maisha yake,” alisema staa mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na ndugu wa Dida.
Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kuolewa huko, Dida alisema safari hii ndoa yake ikivunjika haolewi tena.