Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja |
Jeshi
la Magereza Tanzania Bara limewafukuza kazi askari watatu kwa kosa la
kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo na kwamba watafikishwa
mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Askari
hao watatu wa Magereza ni miongoni mwa watu saba walikamatwa na na
Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati, kwa kushirikiana na askari wa
Wizara ya maliasili na Utalii, mkoani manyara kwa tuhuma za kukutwa na
nyara za serikali zenye thamani ya sh. mili. 55.
Taarifa
iliyotolewa na jeshi hilo jana Jijini Dar es Salaam na Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja, imesema kuwa hatua hiyo
inafuatia uchunguzi wa awali kubaini ukiukwaji wa taratibu na maadili ya
jeshi pamoja na sheria za uwindaji wa wanyamapori.
Ilisema
kuwa Julai 23, mwaka huu, maofisa wane ambao ni Mrakibu Msaidizi wa
magereza, Joseph Kimaro, Sajenti Ketto Ramadhani, Koplp Silyvester
Dionice na Warda Richard Barick wa gereza la Kiteto Manyara walikamatwa
na kikosi cha kuzuia ujangili wakiwa na gari la Maereza pamoja na
silaha. Gari hilo lilipakia nyara za serikali.
Kufuatia
tukio hilo, hatua zilizochukuliwa ni kuwafukuza kazi maofisa watatu
ambapo watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Taarifa
imefafanua kuwa Afisa Mrakibu Msaidizi wa magereza, Joseph Kimaro
amefunguliwa mashtaka ya nidhamu na kusimamishwa kazi kwa kosa la kwenda
kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza hadi maamuzi ya mamlaka ya
kinidhamu inayomhusu yeye itakapotoa maamuzi dhidi yake.
Kwa sasa amezuiliwa kituo cha polisi BBabati kusubiri kufikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.
Aidha
taarifa imesema kuwa Mkuu wa Gereza Kiteto, Mrakibu wa magereza Ally
Ramadhani Sauko kwa kutumia madaraka yake vibaya, yeye amevuliwa uongozi
na kuhamishiwa ofisi ya Mkuu wa Magereza Manyara, akisubiri maamuzi ya
mamlaka ya kinidhamu inayomhusu yeye, kufuatia mashtaka ya kinidhamu
yaliyofunguliwa dhidi yake.