Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Washika
bunduki wa kaskazini mwa jiji la London, klabu ya Arsenal, wamefufua
upya mipango ya kutaka kumsajili na kumrudisha tena London nahodha wao
wa zamani na mwanandinga wa wazee wa Katalunya kwa sasa, FC Barcelona,
namzungumzia kiungo Cesc Fabregas katika majira haya ya joto.
Nyota
huyo wa zamani wa Asernal kwa sasa yupo mapumzikoni akila raha na
kuweka akili sawa kufuatia kuwa na msimu mgumu Camp Nou na anapumzika
baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Hispania
iliyoshindwa kutwaa kombe la mabara baada ya kufungwa na wenyeji Brazil
mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.Taarifa
za huko Hispnia zinadokeza kuwa nyota huyo bado ana nia ya kubakia Camp
Nou, lakini bado wasiwasi umetanda kama ataendana na mipango ya
kocha Tito Vilanova, na ikizingatiwa kuwa msimu uliopita alikaa benchi
katika baadhi ya mechi kubwa kwa klabu yake.
Hana furaha? Maisha ya Cesc Fabrega katika klabu yake ya Barcelona yameenda tofauti na mipango yakeEndapo
kiungo huyo ataamua kutoka, Asernal hawatapata shida kumrudisha kwani
wakati wanamuuza kwa pauni milioni 25 kwenda Barca, kulikuwa na
makubaliano kuwa endapo Fabregas mwenye umri wa miaka 26 atakuwa
anaihama klabu hiyo, The Gunners watakuwa wa kwanza kufikiriwa.
Kama
Wakatalunya watamuuza Fabregas, washika bunduki wa London watakuwa
wakwanza kumrejesha nahodha wao kwa usajili wa pauni milioni 25
Hashawishiki? Bosi wa Barca Tito Vilanova amempotezea Fabregas katika michezo mingi muhimu
Wakati
huo huo, washika bunduki wa London wameamua kufufua mipango yao ya
kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams kufuatia Thomas Vermaelen
kurejea katika majeruhi.
Nyota
huyo wa Wales anawindwa sana na Arsene Wenger majira haya ya usajili,
lakini wameshindwa kufikia dau linalohitajika la pauni milioni 10.
Mtandao wa michezo wa Sportsmail.com ulisema
jumanne ya wiki hii kuwa, nahodhaVermaelen atakosa maandalizi ya msimu
mpya kutokana na majeruhi, na ataiacha Arsenal ikiwa na mabeki wazima
wawili wa kati; Laurent Koscielny na Mertesacker.
Majeruhi ya Thomas Vermaelen yanawalazimu Arsenal kuanzisha mbio za kumsaka Ashley Willia
FULL SHANGWE