Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, June 3, 2013

WIZARA YA ARDHI IFUTE SHERIA MRADI WA MJI MPYA WAKIGAMBONI


PROF TIBAIJUKA
  • Si busara kutumia ubabe katika kuchukua ardhi ya wananchi bila Ridhaa yao.
  • Si Uzalendo kuondoa wazawa, ardhi wapewe wageni! 
Wizara ya Ardhi imejikuta kuwa mvunjivu wa sheria za nchi,na kutumia nguvu, na kuwatisha wananchi wa wilaya Temeke  kwa kutaka kuwanyang'anya Ardhi katika kutekeleza mradi wa mji mpya Kigamboni (KDA).
Malalamiko na vilio vya wananchi wa maeneo yanayokadiliwa kuanzia ekari 6,000 hadi 50,000 wilaya ya Temeke,vilio vya wananchi hao ambao wanatishiwa kuondelewa katika makazi au ardhi zao ,vimekuwa vilio vya samaki machozi
yanakwenda na maji.

image24Sura mpya ya kutisha inayowaletea mashaka wakazi  Kigamboni na maeneo mengine ambayo Waziri wa Ardhi Prof.Anna Tibaijuka ametangaza kuwa yatachukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya Kigamboni,wananchi wamekuwa wakijiuliza hivi serikali inaivunja sheria ya nchi kwa kupitia wizara ya Ardhi? na kuwatosa wananchi wake katika wingu la giza!
Utata unakuja pale waziri Anna Tibaijuka anapozitaja kata za Pemba Mnazi, Kisarwe II,Kimbiji, wilaya Temeke,kuwa kata hizo zitachukuliwa ili kuongezea utanuzi wa mradi mji mpya Kigamboni,wakati maeneo ya awali yalio........
tajwa jatika mradi, kata Kimbiji,pemba mnazi,kisarawe II hazikuwepo. Wananchi wa maeneo hayo wanajiuliza maswali mengi ambayo majibu yake hakuna,
Hivi Serikali itachukua ardhi na kuwafukuza wananchi katika maeneo hayo bila ridhaa ya wenye mali au makubaliano? Je ?kufanya hivyo Serikali itakuwa inavunja  "sheria za utwaaji Ardhi Na.47 ya mwaka 1967 na Sheria ya Mipango Mji Na.8 ya mwaka 2007."
Sheria za utwaaji Ardhi sura ya 118 inauhusu upangaji vizuri na ujenzi wa makazi tu na siyo viwanda, maofisi,maghorofa ma tahasisi za Umma! sasa kama sheria ndiyo hii ,Wananchi wa maeneo yaliyotajwa na Waziri Anna Tibaijuka kwa nini waondelewe pale ? harafu wawekwe akina nani?
Sheria hii hairuhusu Serikali kuleta watu wengine ili kuwaendeleza kwa kisingizio chochote kile hata cha uwekezaji. Ardhi ikitwaliwa chini ya sheria hii itagawanywa kwa wakazi walewale waliokuwapo baada ya kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya miundombinu.
Wizara ya Ardhi isijinye kichwa ngumu katika kuvunja sheria hizi na kuwa wasiri wa kuwastukiza wanachi baadala ya kuwashirikisha katika miradi ya maendeleo, 
Sheria ya Mipango Miji Na.8 ya mwaka 2007 hisitumike kama mwanya wa kuwanyang'anya Ardhi wananchi na kuigawa na itakayobaki kuwapa marafiki au wawekezaji,kufanya hivyo ni kuwadhurumu wapiga kura na wananchi wa maeneo usika. ni vema taratibu za kisheria zifuate kuliko Wizara Ardhi kutumia Ubabe.kwa sababu kifungu namba 8 cha sheria hiyo kinataka kabla ya kutangazwa eneo kuendelezwa lazima wananchi waitwe na waelezwe na kukubali mpango au mradi huo.  Kinyume cha ni kuvunja sheria
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...