Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, June 13, 2013

WAZIRI NCHIMBI AFUNGA MAFUNZO YA NGAZI YA JUU YA MAAFISA MAGEREZA, JIJINI DAR ES SALAAM

PIX 1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikagua gwaride la wahitimu kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi ngazi za juu kwa maafisa wa Magereza. Sherehe hizo zimefanyika katika chuo cha maafisa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.PIX 2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Hamza Abdalla kwa niaba ya wahitimu wa kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi ngazi za juu kwa maafisa. Sherehe hizo zimefanyika katika chuo cha maafisa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.PIX 3Gwaride la wahitimu kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi wa ngazi za juu kwa maafisa wa magereza likipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani). Dk Nchimbi aliyafunga mafunzo hayo katika chuo cha maafisa wa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
PIX 4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na askari na maafisa magereza kabla ya kufunga mafunzo ya Uongozi wa ngazi za juu kwa maafisa wa magereza kozi namba 20 ya mwaka 2013. Sherehe hiyo ilifanyika katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...