Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, June 13, 2013

Mario Balotelli amvisha pete ya uchumba mpenzi wake Fanny

Balotelli & Fanny
Kuachana na kurudiana ni sehemu ya mapenzi, kama huamini muulize mcheza mpira wa timu ya A.C Milan Balotelli! ambaye inasemekana hivi karibuni amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Fanny Neguesha, yule yule aliyewahi kutamka angewaruhusu wachezaji wote wa Real Madrid walale naye endapo wangeweza kuwatoa Borussia Dortmund katika UEFA Champions League.

Jumamosi iliyopita (June 8) Fanny mwenye miaka 22 alipost picha katika akaunti yake ya instagram inayoonesha kidole chake cha mkono wa kushoto kikiwa tayari kimewekewa uzio (pete) ya uchumba iliyosindikizwa na caption hii “It official… like me.” Balotelli na fanny wamekuwa katika mahusiano kwa muda wa miezi 6 sasa.
Fanny engagement ring
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail inasemekana pete hiyo ya diamond ina thamani ya £100,000 ambayo ni zaidi ya Tsh 250,000,000 ambayo ukiongeza M 50 tu inaifikia zawadi ya BBA ‘The Chase’, LOL! People have money.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...