Watanzania
60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini
humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani.
Rais Obama amewasili Afrika Kuisini juzi kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal.
Watu
hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika
Kusini. Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama
wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri hatua za kisheria zaidi.
Ofisa
mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema
Watanzania hao walirejeshwa nchini jana na kwamba hivi sasa wanasubiri
sheria kuchukua mkondo wake.
“Safisha
safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika
Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa
huyo.
Hivi sasa Rais Obama yupo Afrika Kusini akiwa ameongoza na mkewe Michelle Obama na watoto wao wawili; Malia na Sasha.
Kesho Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.




