Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
WAFANYAKAZI
wa Supermarket ya Nakumatt, iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro,
wameulalamikia uongozi wa duka hilo kwa madai ya kuwanyanyasa na
kuwaomba rushwa ya ngono.
Wafanyakazi
hao ambao tayari walishafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Leonidas Gama walidai wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya
unyanyasaji ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono na Meneja Mkuu na na
msaidizi wake.
Walisema
imekuwa kawaida kwa kila msichana anayefika kuomba nafasi kazi, lazima
aombwe rushwa ya ngono huku wanaume wakitakiwa kinyume na maumbile: “Kila
msichana anaefika hapa kuomba nafasi ya kazi, anaombwa rushwa ya ngono
ndipo apatiwe kazi huku wanaume wakiingiliwa kinyume na maumbile,” walisema.
Aidha walisema sababu iliyowafanya wafikie maamuzi ya kuandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa
kutaka msaada ni kukithiri kwa vitendo hivyo.
Akizungumzia tuhuma hizo, Meneja wa Nakumatt Moshi, Alfrick Milimo
alikanusha tuhuma hizo na kudai kwamba zote hizo ni njama za kupakana
matope za watu wasiolitakia mema duka hilo.
Alisema kumekuwa na watu wanaozunguka kuwashawishi wafanyakazi huku
akikumbushia matatizo yalitokea kipindi cha nyuma kati ya uongozi na
wafanyakazi wake na kuwa tayari wameshabaini njama hizo.
Alisema katika duka lake kuna wafanyikazi wa Kenya na Tanzania lakini
mara nyingi tatizo linatokea pale wanapowalazimisha Watanzania kufanya
kazi maana wengi hawapendi kufanya kazi bila kushurutishwa:
“Niko hapa
kwa ajili ya kuwafundisha, kuwaonya na kuwaelekeza lakini inaonekana
kuwa unapofanya hivyo unaonekana kuwa wewe ni mbaya na wanafika kazini
na mavazi yasizoendana na maadili ya kazi pia wanasinzia
kazini,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amekiri
kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wafanyakazi hao na kuahidi
kuyashughulikia.
Alisema
tayari ameshaagiza Idara ya kazi kulifuatilia suala hilo kwa karibu na
kutoa taarifa mapema ikiwa ni pamoja na idadi kamili ya Watanzania na
Wakenya wanaofanya kazi katika duka hilo.
Credit: Audiface jackson blog