Wahabeshi
18 na raia mmoja wa Kenya wakiwa makao makuu ya idara ya Uhamiaji
mkoani Tanga ambapo walikuwa wakiandaliwa mashitaka kabla ya kufikishwa
mahakamani Jumanne wiki hii kwa kuingia nchini bila kibali. Picha na
Mashaka Mhando, Tanga
Na Mashaka Mhando,Tanga
IDARA ya Uhamiaji mkoani Tanga, inawashikiliwa raia 18 kutoka Ethiopia na raia mmoja wa Kenya, kwa kuingia nchini bila kibali.
Ofisa
Uhamiaji wa mkoa wa Tanga, Bw. Sixtus Nyaki, alisema ofisini kwake
kwamba raia hao, walikamtwa Juni 9 mwaka huu, kwenye nyumba moja eneo la
Sahare katika Jiji la Tanga.
Alisema
idara yake ilipata taarifa kwamba kuna nyumba moja ya Mtanzania mwenye
asili ya Pemba, alikuwa amewahifadhi watu wengi kwenye chumba kimoja na
hivyo maofisa Uhamiaji wakiongozana na askari polisi, waliwakuta wakiwa
wamejibana kwenye chumba hicho kilichokuwa na kitanda kimoja.
Hata
hivyo, Ofisa huyo hakuwa na maelezo zaidi kuhusu watu hao ambao hawajui
kuzungumza Kiingereza zaidi ya Kihabeshi, hawajapata taarifa kujua
wametumia usafiri gani kufika hapa nchini na wanaendelea na uchunguzi
kujua hali hiyo.
Inaaminika
kwamba Wahabeshi hao wametumia usafiri wa majahazi kutokea Mombasa
nchini Kenya na wamehifadhiwa hapo ili waweze kutafutiwa usafiri
mwingine kwenda Afrika Kusini ambako huko wamekuwa wakitafuta nafasi za
kwenda nchi za Ulaya na Amerika.
Wimbi
la Wahabeshi kuingia nchini hasa kupitia katika mkoa huu wa Tanga
limeshika kasi zaidi kutokana na kuelezwa kwamba raia wamekuwa wakipita
kutokea nchini Kenya kwenda Afrika Kusini kutafuita maisha.
Mwishoni
mwa wiki Wahabeshi wengine wapatao 26, walimaliza vifungo vyao vya
miezi mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini bila
vibali na idara hiyo iliwasafirisha kurudi makwao.
Wahabeshi
hao walikamatwa katika eneo la kizuizi cha polisi Kabuku, wakiwa
wamepakiwa kwenye kontena la lori hivyo wakati wakipita hapo polisi
walisikia sauti za watu wakitaka kutoka ambapo walipolifungua waliwakuta
Wahabeshi hao ambapo wengine sita walikutwa wamekufa kwa kukosa hewa.
Credit: Pamoja Blog