|
Hapa Jackline wolper akikaribiswa chakula na kusema kashiba |
Msanii wa filamu nchini tanzania jackline masawe wolper amesema
hategemei wanaume kama ambavyo marafiki zake na jamii walivyomkariri.
Jack ameeleza kuwa yeye si mwanamke tegemezi ndio maana ameweza kumiliki
kampuni yake mwenyewe ya filamu na biashara kibao ndani na nnje ya mkoa
huu wa dar,Mwanadada huyo aliyasema hayo huku akidai anashangazwa na
habari kuwa mwaka huu hana mwanaume ndio maana haonekani akifanya fujo
mjini,jambo amabalo yeye anaona ni kituko kwani badala ya watu kufikiria
au kumshauri awe na majumba makampuni makubwa wao wanataka kumuona jack
wa mashoping na mastarehe kitu ambacho mwanadada huyo anasema kwasasa
hayupo tiyari kwani ameshakuwa na ana majukumu mbele yake.
|
Hapa
akiwaza jinsi ya kujibu maswali picha hizi ni ndani ya kampuni ya
bwana ray na johari iliyopo sinza ni ndani ya RJ Company tulipomkuta
msanii huyu |
Akipiga stori na mwandishi wa thesuperstarstz jack alisema hana haja ya
kupigizana kelele nao wanaojifanya kumjua wakati hawamjui ki hivyo
kwani ana amini katika hii dunia kila mmoja ameletwa kwa kazi maalumu na
hawezi kumuingilia mtu,,,
Nashangazwa
na watu wanaojifanya kunijua kiundani wakati hawanijui kihivyo mimi
ninamaisha yangu na sina muda wa wakupiga soga na watu wasiokuwa na la
kufanya.
|
Hapa ni moja ya pozi la mwanadada huyu
|
Mwanadada huyo ambaye kwa sasa inasemekana ndio taa ya mabinti sokoni
kwani amesema kwasasa yupo kwenye mipango ya kushusha bonge la mjengo na
kuwataka mashabiki zake waendelee kumuunga mkono kama ilivyo sasa,Na
kuhusu kazi Jack anasema anamshukuru mungu kwani kafanikiwa vizuri sana
nakusema kiutani kuwa ukitaka kujua jack ninani nenda kwa wauza cd
watakuambia
|
Hapa akitaka kuaga mara baada ya kumaliza kilichompeleka katika ofisi za Rj Company |
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake wa sasa jack alisema nadhani kwa sasa
sintokuwa tiyari tena kwani naogopa maisha haya kila nikipata mtu wangu
wajanja wanabeba na mimi kazi ya kugombea mabwana mwenzenu siwezi
kabisa,,,ila kwa sasa nikimpata nitahakikisha hadi watu wakimjua basi
tiyari kashakuwa mume wangu alisema jack mwanadada mpole na mwenye
tabasamu kila akiongea.
Thesuperstarstz inamtakia kila la kheri katika safari yake hiyo