Mtafiti
wa Masoko ya Ajira, VETA Makao Makuu Julius Paul Mjelwa akitoa maelezo
kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya
Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), kuhusu huduma na mafunzo
mbalimbali yanayotolewa na vyuo vya VETA.
Mhandisi
Adrian Kashula wa VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, akitoa maelezo
kuhusu teknolojia ya kisasa ya umeme wa viwandani ambayo inatumia eneo
dogo na kutoa taarifa pale panapotokea hitilafu, akitoa maelezo kwa
wageni waliotembelea banda hilo.
Mwanafunzi
wa Mwaka wa Tatu wa VETA Chang’ombe Dar es Salaam, fani ya uchoraji
ramani na usanifu majengo, Fatma Mohamedi akitoa maelezo kuhusu mafunzo
ya taaluma hiyo yanayotolewa na chuo hicho katika ngazi mbalimbali.
Baadhi
ya mashine na mitambo inayozalishwa na vyuo mbalimbali vya VETA nchini,
ambayo ikitumika vema inaweza kulikomboa taifa kiuchumi kwa kuepuka
utegemezi wa mashine na mitambo kutoka nje.
Matumizi
ya dezeli na petrol kuzalisha umeme kutumia jenereta sasa basi. VETA
imekuja na teknolojia ya kuzalisha umeme kwa kutumia betri, hivyo
kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya dizeli na
petrol. Mwanafunzi wa VETA wa Mitambo na Mashine, Emmanuel Ngowo
akionyesha jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Kwanini
tunedelea kuuza ngozi ghafi nje? VETA wamekuja na jibu kupitia Chuo
chao cha Dakawa, Morogoro kinachotoa mafunzo ya usindikaji na uzalishaji
wa bidhaa za ngozi vikiwemo viatu vya aina mbalimbali. Mwanafunzi wa
VETA Onesmo Mrisho akitoa maelezo jinsi wanavyozalisha bidhaa za ngozi.
Hawaamini,
kisha wakafurahi baada ya kupata maelezo kuhusu mafunzo ya hoteli na
utalii yanayotolewa na vyuo vya VETA vya Dodoma na Njiro mkoani Arusha.
Pichani Mwanafunzi Theopista Michael akitoa maelezo wa wageni
waliotembelea banda la VETA katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya
Dar es Salaam.
Unajua
mvinyo upi unakwenda na chakula kipi? Tembelea banda la VETA, Sabasaba
upate maelezo ya kutosha. Pichani Mwalimu Theonestina Raphael wa VETA
Njiro, Arusha akielezea mvinyo Mwekundu na vyakula unaoendana navyo.






