Ni
majanga kwa kwenda mbele kwa Top in Dar. Staa huyo aliyepiga show ya
nguvu weekend hii jijini London, Uingereza ameibuka na kusema kuwa
promota wa show hiyo, Victor aka Dj Rule amemuacha kwenye mataa baada ya
show. TID alitumbuiza pamoja na Jaguar wa Kenya.
Kupitia Facebook, TID ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohamed ameandika:
“My mind is not some stupid promota is trying to rob me,am not goin
to let it happen am calling my balozi why a Kenyan artist
hajamzingua……ndo maana hatuendelei. DJ rule victor amekimbia hela zangu
hajanipa left me in a hotel hang in like a fan.”
Jitihada za kumtafuta Dj Rule azungumzie suala hili zimegonga mwamba kutokana na kutopokea simu yake.
Hata hivyo Dj Victor aliandika kuwa show hiyo ilifanikiwa kwa kiasi
kikubwa na kumpongeza TID kwa kwenda kwenye show siku chache tu baada ya
kumzika Mangwea.
“The East African Superstars at the sold out TID & Jaguar last
night at the Ville London thanxs mostly to TID who made it at last after
his dear friend passing on few days ago.”