“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 06. 2013.
WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA VIFO.
 MNAMO 
TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO VWAWA 
BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.840 BKD 
AINA YA TOYOTA HARRIER LIKIENDESHWA NA DEREVA BROWN S/O MWAKIBAMBO,MIAKA
 34,KYUSA, MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O 
HALINGA,MIAKA 27,MKULIMA MKAZI WA ILOLO AKIWA  AMEMBEBA MTOTO WAKE 
AITWAE HELENA D/O SAMSON,UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU, KYUSA  NA 
KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA 
HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI . TARATIBU 
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA 
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
 BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA KYELA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO 
TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA 
WAGENI IITWAYO GWAKISA ENEO LA KYELA - KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA 
MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. LUKINDO S/O JOHN,MIAKA
 45 NA 2. MSEMAKWELI S/O JOHN, MIAKA 27 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI 
RWANDA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU ILIYOTUMIKA NI 
KUSAFIRI KWA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA 
UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI 
DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA 
MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA ZA 
KISHERIA  DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.
Signed By,
 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
 





 
 
 
