TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati
ya msiba tunaomba kutoa ya taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert
Mangweha hautoweza kufika siku ya Jumapili ya tarehe 2/06/2013 kama
ilivyo taarifiwa hapo awali, hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya
uwezo wetu.
Kwa sasa
tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu waliopo
nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha
zaidi.
Tunaomba radhi Watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu kwa hili.
Asante
Mwenyekiti wa Kamati
Kenneth Mangweha