Akichonga na paparazi wetu juzikati jijini Dar, Jack alisema kwa sasa
yeye na kuzaa mbalimbali kwa vile ana mipango mingi ya maisha ingawaje
anapenda sana watoto.
“Napenda sana watoto lakini sitarajii kabisa kuzaa kesho wala
keshokutwa, kwasababu ni lazima ujipange sawasawa ili uweze kumtunza
vyema mtoto pindi utakapojifungua,” alisema na kuongea:
“Wanawake wengi wanaharakisha kuzaa matokeo yake ni kuwaacha watoto
nyumbani na mahausigeli wakiwa wadogo ili wao wakatafute chochote,
lazima ukae na mwanao hata mwaka mmoja aweze kupata malezi bora ndiyo
maana nasema lazima ujipange sana.”




