MSANII wa
filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa
anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga
pamoja na watoto.Akizungumza na
mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli
kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa
wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na
mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye
mazishi yake.Alisema
sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla
hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku
ya mazishi lazima wakumbuke fadhila.
“Unajua
kufa ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu watakaokuwa wengi ni
watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama yao, wengine ni
waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki,”alisema Aunty Lulu.