Wawili hao waliokuwa wanaelekea nchini Nigeria kutoka Brazil, walikuwa
wamemeza vidonge 54 vyenye Cocain lakini baada ya kuwekwa chini ya
uchunguzi wa polisi wakaweza kuvitoa vidonge hivyo.
Wawili hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta mjini Nairobi wakitoa Brazil kuelekea mjini Lagos, Nigeria.
Asubuhi ya leo walipelekwa katika mahakama moja mjini Nairobi na
kushtakiwa kwa kosa la kumiliki madawa ya kulevya ambayo ni haramu
nchini Kenya.
Ni wiki hii tu ambapo mzozo wa kidiplomasia umekuwa ukitokota kati ya
Nigeria na Kenya baada ya kufurushwa kutoka nchini humo kwa
mfanyabiashara mwenye utata raia wa Nigeria Anthony Chinedu baada ya
kuhusishwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Chinedu alirejeshwa Nigeria kufuatia amri ya rais wa nchi hiyo Uhuru
Kenyatta kuwa raia wa kigeni wanaohusika na biashara haramu za madawa ya
kulevya wurejeshwe kwao.
Hata hivyo mzozo ulianza pale ndege ya Kenya iliyokuwa imewabeba maafisa
wa Kenya waliokuwa wanamrejesha Chinedu nchini Nigeria ilipozuiliwa
katika uwanja wa Ngege wa Murtallah baada ya kumfikisha Chinedu
nyumbani.
Kwa sasa juhudi za kidiploamsia zinagli zinaendelea kuweza kuwarejesha
Kenya maafisa hao. Maafisa wa Nigeria wamezungumzia mzozo huo
wakikanusha madai kuwa maafisa wa Kenya waliteswa
chanzo:bbc