Mkurugenzi
wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akirejea
kwenye meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa
mafunzo hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
Kikosi hicho kikitembea kwa ukakamavu kabisa kusonga mbele tayari kwa kutoa heshima zao kwa wageni rasmi.
Mkurugenzi
wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akipokea
heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya
kukabiliana na ujangili katika hifadhi za Taifa,kulia ni Katibu Tawala
wa Mkoa wa Iringa bwa.Adam Swai na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa
TANAPA,Bwa.Martin Loiboki.
Mkurugenzi
wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akimkabidhi
cheti cha kuhitimu mafunzo hayo ya Uaskari,Frank Anthon Malema,pichani
kulai ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA,Bwa.Martin Loiboki na kushoto ni
Mkufunzi wa Mafunzo hayo na Mhifadhi wa TANAPA,Bwa.Genes Shayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Elisamehe
Elisafi Mdeme kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na
kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi
akimpongeza John Kijazi baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo
hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.Martin
Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa
maelezo kwa Allan Kijazi Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa
TANAPA wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji
wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha
Nation Park. Askari
maalum wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili katika hifadhi za
taifa wakionyesha moja ya kazi zao wakati wakitafuta majangili katika
hifadhi hizo Mmoja wa Askari wa kikosi hicho akilenga shabaha Mkufunzi
wa Mafunzo hayo Martin Mthembu akielezea mafanikio ya kikosi hicho
katika kulenga shabaha kwa mkurugenzi wa hifadhi za taifa TANAPA Ndugu
Allan Kijazi wa pili kutoka kushoto wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi
wa Uhifadhi Martin Loiboki na wa kwanza kushoto ni Dr. Christopher
Timbuka Mhifadhi Mkuu Ruaha Nation Park Mkufunzi
Martin Mthembu akielezea jinsi askari hao wanavyotakiwa kuwatafuta
majangili huku wakiwa na maamuzi ya haraka bila kuchelewa na kutoua
jangili ambaye hana madhara askari wa anatakiwa kufanya kazi yake kwa
ufanisi lakini pia kulinda usalama wake yaani fanya kazi yako lakini
rudi salama Askari mwanamke pekee Aikande Lema akilenga shabaha huku mkufunzi huyo akiangalia Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi naye akimshuhudia askari huyo Askari Aikande Lema akirejea mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na mwalimu wake kwa mafanikio katika kulenga shabaha.