Na Benedict Liwenga, Maelezo.
WASANII
wa filamu nchini wameshauriwa kuwasilisha miswada ya filamu kwa Bodi ya
Filamu ilkaguliwe na kupewa kibali kama unafaa,umefata sheria na
haujakiuka maadili ya sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza pamoja na
kanuni zake.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bi.Joyce Fissoo wakati wa kikao na mtengenezaji wa filamu Aunt Ezekiel
kuhusiana na kazi yake mpya ijulikanayo kama Scola.
Katibu
huyo amefafanua kuwa kuna umuhimu wa wasanii kufata sheria na taratibu
za filamu kabla ya kuanza kutengeneza na kuzitoa filamu zao ambapo
sheria inawataka kuwasilisha miswada (script) Bodi ya filamu ili
ukaguliwe na kupewa idhini yakuendelea na kazi hiyo.
“Wasanii
mnatakiwa kuzingatia sheria na kuwasilisha script ili zikaguliwe na
kupata ruhusa kwa mujibu na taratibu za sheria kabla ya kuanza
kutengeneza filamu kwa sababu sheria Na 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na
Michezo ya Kuigiza pamoja na kanuni zake zinataka wasanii kutotoa au
kutengeneza filamu kabla ya kupeleka mswada(script ) kwa Bodi.
Aidha
Katibu huyo amefafanua kuwa wasanii wanapotengeneza picha kupitia
script ambazo hazijakaguliwa kuna uwezekano mkubwa wakuwepo sehemu
ambazo zinakiuka maadili ya mtanzania,ikiwepo uvaaji wa mavazi mafupi
yaliyopitiliza kwa waigizaji wanawake,lugha mbaya na baadhi ya vitendo
vingine visivyofaa kuoneshwa kwa umma.
Bi
Fissoo amesema kuwa Bodi imepewa mamlaka kwa mujibu wa Shetia kuzuia
filamu hizo ambazo hazijakaguliwa ,na kama msanii hajafuata sheria
atapata hasara kutokana na gharama ambazo atakuwa ametumia na endapo
filamu hiyo itafutwa, jambo a,balo Bodi isingelipenda liwakute wadau
wake.
Kwa
upande wake Msanii wa Filamu za Kiswahili Aunty Ezekiel ameomba radhi
kwa kutoleta script yake ya filamu hiyo mpya ya SCOLA Bodi ya Filamu na
ameahidi kurekebisha baadhi ya vipengele kama alivyoelekezwa na Bodi
hiyo kwani vitu hivyo vinaweza kurekebishika.
Aunty
Ezekiel amefurahishwa sana na kuishurukuru Bodi ya Filamu Tanzania kwa
kufanya majadiliano mazuri juu ya filamu yake kwa kubaini mapungufu
yaliyopo na ameahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha filamu hiyo na pia
amewaasa wasanii wengine wote kuwa na imani na Bodi ya Filamu na
kutokuwa na dhana tofauti juu ya Bodi hiyo.
Aunty
Ezekiel ni msanii aliyetengeneza filamu nyingi hapa nchini ambazo
zinasambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment iliyopo hapa nchini.
Credit: Mdimu Blog