MKE wa naibu wa chifu
katika wilaya ya Marigat Alhamisi aliaga dunia katika hali isioeleweka baada ya
mumewe kumpata akinywa pombe haramu ya chang’aa katika nyumba ya
jirani.
Naibu wa chifu wa kata ya
Arabal Bw William Yegon inasemekana hakufurahia pale alipompata mkewe Bi Mary
Kobilo, 46, akipiga mtindi na wanakijiji wengine.
Wenyeji walioongea na
Taifa Leo walisema kuwa wawili hao walianza kuzozana wakati wa tukio hilo la saa
kumi na mbili jioni Jumatano huku naibu huyo wa chifu akimlaumu mkewe kwa
kumwaibisha kwa kunywa pombe hiyo haramu ilhali yeye alikuwa afisa wa serikali
anayefaa kuongoza vita dhidi ya pombe haramu.
“Naibu huyo wa chifu alikasirishwa sana kwamba mkewe alikuwa
akimkosea heshima licha ya serikali kutangaza vita kwa wapikaji wa pombe
haramu,”alisema mmoja wa wanakijiji ambao hakutaka kutajwa
jina.