Rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa hospitalini kwa siku
ya nne ambako anapokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu.
Duru
kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, zinasema kuwa Mandela mwenye umri
wa miaka 94, yuko katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa.
Jamaa zake pamoja na aliyekuwa mkewe Winnie Madikizela-Mandela, walimtembelea hospitalini Jumatatu
Mwanawe
Mandela Zenani (Mandela-Dlamini), pia alirejea kutoka nchini Argentina,
ambako yeye ni balozi.Serikali imekuwa ikisema kuwa hali ya Mandle
inatia wasiwasi ingawa madaktari wameweza kuidhibiti.Amekuwa katika
chumba ya wagonjwa mahututi tangu kulazwa hospitalini Jumamosi kwa mara
ya tatu mwaka huu.Mwezi Disemba , bwana Mandela alilazwa hospitalini kwa
siku 18 baada ya kupata maradhi ya mapafu,Kumekuwa na taarifa za
simanzi kwa mara ya kwanza huku familia yake ikikusanyika kando yake,
baadhi ya watu wakisema kuwa ni muda wamwache Mandela aende zake.
Bwana
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi
, ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa
mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini
Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu. Msemaji wa
serikali Mac Maharaj amesema kuwa maafisa katika hospitali wanataka
kudhibiti idadi ya watu wanaozuru hospitali hiyo ili wampunguzie bwana
Mandela usumbufu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa
mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito
wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu
anapougua.
Lakini
mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna
matumaini madogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi, huenda akapona.
Anasema
kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema
kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa
jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa
akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela. Chanzo:
bbcswahili