Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, June 3, 2013

Jacky Wolper, Izzo B na Hemedy PHD ndani ya movie moja ‘My Princess’

My-Princess
Waigizaji wa filamu Jacqueline Wolper na Hemed PHD, wameigiza pamoja na rapper Emmanuel Simwinga aka Izzo B kwenye filamu iitwaayo My Princess.

Katika movie hiyo Hemed na Jacky Wolper ni wapenzi ambao bado ni wanafunzi wa chuo. Lakini Izzo Business na yeye anampenda sana Jacky Wolper. Jacky anapata mimba ya Hemed na kulazimishwa kuitoa na baadaye kupata matatizo mengine yanayopelekea kutaka kukatwa mguu.
Movie inaendelea na baadaye anapona kwa dawa za asili akiwa kijijini ambapo Hemed hakwenda hata kumuangalia, lakini Izzo Business kutokana na mapenzi mazito yaliyomzidia kwa kwa Wolper,aliulizia na kumfatilia hadi huko kijijini na kumshagaza Wolper kwamba amefikaje kule.
Baada ya kupona na muda mrefu wa Hemed kutokumuona Wolper…anashanga kumuona Wolper akimshangilia Izzo Business akicheza basketball na baadaye wakisepa wote kama wapenzi.Kuna visa vingi humu ndani kuhusu Izzo Business ndani ya Cassino,Music,Love,Basketball na vingine kibao kwenye story tamu ya My Princess. (Source: www.bongomoviestz.com)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...