Italia imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la
Mabara baada ya kuichapa Uruguay kwa mikwaju 3-2 ya penalty.
Mechi hiyo imemalizika kwa dakika 120, timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Italia ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Astori katika dakika ya 24, Cavani akaisawazisia Uruguay katika dakika ya 58.
Ilipowadia dakika ya 73, Italia wakatangulia kwa mara ya pili kwa bao lililofungwa kwa mkwaju wa faulo na Diamant lakini Cavani tena akajibu katika dakika ya 78 kwa mpira wa faulo pia.



