Mwigizaji mkongwe na mahiri katika tasnia ya filamu Nchini single
Mtambalike ‘Richie’ ameachia filamu kali na ya kusisimua ya Safari,
filamu hiyo ambayo imeteka soko la filamu Bongo na inafanya vizuri kazi
yenye ubora huku ikishirikisha wasanii wenye uwezo katika tasnia ya
uigizaji filamu ya Safari imeingia jumatano wiki hii.
“Mara nyingi sikurupuki katika kutengeneza filamu kitu ambacho kimenifanya nitumie muda muda mwingi katika utayarishaji wa kazi zangu, nimekuwa makini ili kukidhi haja kwa wapenzi wa filamu nchini ambao wanamjua Richie akitoa filamu inakuwa na mafundisho katika jamii,”anasema Richie.
Filamu ya Safari ni kisa cha aina yake kinachohusu kundi la vijana waliokuwa safarini na kukutana na maajabu yanayosambaratisha kundi hilo, ni filamu nzuri inayofundisha na kuburudisha, filamu hiyo imeshirikisha wasanii nyota kama Chuchu Hans, Zagamba,Irene Uwoya, Richie na wasanii wengine nyota katika tasnia ya filamu.