![]() |
Mh. J.M.Kikwete -Mwenyekiti wa CCM Taifa |
MLIPUKO wa bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa kufunga
kampeni za udiwani kwa CHADEMA mkoani Arusha na kuua watu wanne,
umeiweka kwenye wakati mgumu serikali ya CCM, Jeshi la Polisi na Bunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema juzi bomu lililolipuliwa katika
mkutano wa CHADEMA ni la kijeshi na limetengenezwa China na uzoefu
unaonesha hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na
maadui vitani.
Wakati Pinda akitoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa CHADEMA
wamelihusisha Jeshi la Polisi na tukio hilo huku wakidai wanao ushahidi
unaonesha askari aliyevalia sare akilirusha kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii, wamelidokeza Tanzania Daima
kuwa kukiri kwa serikali kuwa bomu hilo limetengenezwa China, inapaswa
iibane nchi hiyo ieleze iliyemuuzia na alivyoliingiza nchini.
“Kwanini isiundwe tume huru nchini ili nchi ya China iulizwe baada ya
kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Na kama haikuiuzia serikali, basi
ni dhahiri tuiulize China kwanini inafadhili vikundi vya kigaidi nchini
kwetu?
“Je, kama bomu lilitengenezwa China, tuangalie kama mkataba wa majukumu
ya mataifa duniani kuhusu silaha, nchi hiyo inatakiwa kutoka na kauli
kuhusu bomu hilo na kwa kukaa kimya maana yake wanakubaliana na maelezo
ya serikali,” alisema.
Wakati maswali hayo yakionekana kuumiza vichwa vya watawala, viongozi wa
CHADEMA kwa upande wao wamegoma kutoa ushahidi walionao kwa Jeshi la
Polisi mpaka Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji
itakayosikiliza ushahidi huo na kuendesha kesi hiyo.
Hali ya mambo ikiwa hivyo, viongozi wa CCM na wabunge wameanza kulitumia
Bunge kukishambulia CHADEMA kuhusu mlipuko huo kwa lengo la kukinusuru
chama chao, Tanzania Daima limedokezwa mbinu hiyo.
Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa
Ghasia, juzi bungeni walidai kuwa CHADEMA ndio wamekuwa wakihusika na
vurugu zote zinazohusisha mauaji nchini.
Kauli za viongozi hao zinakuja takriban siku tano tangu Katibu wa
Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye, kudai CHADEMA kiliandaa na kuratibu shambulio hilo ambalo
lilitokea kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani.
Licha ya Mwigulu kujadili jambo lililokuwa nje ya mjadala wa bajeti na
linaloendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi, Spika wa Bunge, Anne
Makinda, alimwacha aendelee kukilaumu CHADEMA ikionekana ni mkakati
rasmi wa kulinasua Jeshi la Polisi na serikali ya CCM kwenye tuhuma
hizo.
Katika madai yake, Mwigulu alianza kusema kuwa jambo la usalama wa nchi
hii amekuwa akiliongelea kwa haraka haraka, hivyo watu wamekuwa
hawamwelewi.
“Leo naomba nilisema kwa utaratibu, jambo la usalama nimekuwa nikilisema
na kuomba kama Elia aliyemwambia mtumishi wake kuwa anamwombea Mungu
amfungue macho ya kimungu ili aone jinsi yeye anavyoona.
“Jambo limetokea kama hili la Arusha, nimeyaongea sana mambo haya na
sasa hivi ilipotokea mimi nitasema tena na wenzetu nikiwasema mara
wanasema wataenda jimboni. Nawashauri wasiende tu jimboni, bali wajenge
kabisa makao makuu ya chama chao,” alisema.
Mwigulu ambaye alikuwa akishangiliwa na baadhi ya wabunge na baadhi ya
mawaziri akiwemo William Lukuvi, George Mkuchika, Ghasia, Mary Nagu na
wengine alisema anausema ukweli.
“Ni lazima tuwaze tuvuke mipaka, kuna mambo yanawezekana kabisa yakawa
yamejificha pale. Watu wanaangalia, wanaojitoa ufahamu wanafikiria CCM
inaweza kushiriki.
“Mimi niwaambie CCM, hata bila kushiriki, moja kwa moja inawekwa kwenye
lawama, jambo kama hilo likitokea. Ila CCM haina ushiriki katika jambo
kama hili kwa sababu ndio watu wake kupitia serikali yake inatakiwa
kuwahakikishia usalama,” alisema.
Alisema kuwa ni lazima waangalie maana wengine waliojaa ushabiki
linapotokea jambo wanakwenda moja kwa moja kuwa inawezekana CCM
imeshiriki.
Mwigulu aliongeza kuwa lazima yaangaliwe mazingira ya nchi kwa sasa,
hasa kipindi hiki ambapo wanakuja wageni wakubwa wakiwamo marais wa
China na Marekani, kwamba mataifa mengine ambayo yanajua ujio wa wageni
ni biashara, wanaweza kuichafua Tanzania.
“Sisi tunakimbilia tu CCM ndiyo imejaa midomoni mwa watu, lakini hoja
nyingine Tanzania imekuwa kisiwa cha amani, hivi wale ambao hawatutakii
mema hamjajua eneo wanaloweza wakagusa?” alihoji.
Huku akinukuu ripoti ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kuhusu
utekwaji wa Mwenyekiti wake, Absalom Kibanda, katibu huyo alidai CHADEMA
imetajwa kuwa ndiyo inahusika na matukio hayo ya utekeaji kwa
kushirikiana na maofisa usalama wasio waadilifu ili kuonesha kuwa CCM
imeshindwa kuongoza na sasa inaua watu wake.
“Niliwahi kulisema hili kuwa kuna mambo mengine yanafanyika kwa hujuma
na tumeziona hizo hujuma lakini watu wengine wanawahi kuamini haraka.
“Lakini hawa wenzetu kama waliwahi kumvalisha raia sare za jeshi na
alihukumiwa, wanashindwaje kila wakati wanasema polisi… polisi.
Tunashindwaje kuamini kama wanaweza kumvalisha mtu nguo za polisi na
akafanya yale?” alihoji.
Mwigulu alisema taarifa ya Polisi Mkoa wa Morogoro kuhusu tukio la kifo
cha kijana Ali Zona, kilichotokea wakati wa maandamano ya CHADEMA,
zinasema chama hicho ndicho kilihusika.
“Yule kijana aliyeuawa Morogoro taarifa zilizopo hakuuawa na polisi, ni
CHADEMA wao wenyewe walitoka pale wakatengeneza ile vurugu wakamfyatulia
risasi ili kutengeneza kwamba serikali ya CCM inakandamiza wapinzani,”
alisema.
Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi aliongeza kuwa hata
video ya mauaji ya Arusha iliyowekwa kwenye mtando wa You tube inaonesha
wazi kuwa yalipangwa.
“Yule aliyekuwa anachukua video eti hakushtushwa kabisa na lile bomu,
aliendelea kufuatilia kama vile ni mkanda wa harusi. Iliwahi kutokea
wapi mchukua video kwenye mkutano wa hadhara kitu ambacho hakikupangwa
kimelipuka, kinaua watu, yeye anendelea kama anachukua ‘sendoff’?”
alihoji.
Baada ya Mwigulu kumaliza, Hawa Ghasia ambaye ni mjumbe wa NEC alipewa
nafasi ya kuchangia bajeti hiyo kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge,
lakini naye akatumia muda mwingi kuilaumu CHADEMA kwa matukio ya vurugu
nchini.
Ghasia alitumia muda huo kupanda mbegu ya ubaguzi wa kimaeneo akidai
kuwa CHADEMA wamechochea vurugu Mtwara, Mwanza, Mbeya, Morogoro na sasa
Arusha ili maeneo hayo yasipate maendeleo kama Mkoa wa Kilimanjaro
wanakotoka baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho.
Ghasia alisema wiki iliyopita alikuwa Kilimanjaro anakotokea Mbowe na
Ndesamburo, hakuona vurugu za kuchoma matairi wala kupigwa kwa mabomu
kama ilivyo Arusha.
“Jamani tuwe macho na hawa CHADEMA hawataki wawekezaji waende mikoa
mingine tofauti na Kilimanjaro ndiyo maana wanahamasisha vurugu katika
mikoa ya wenzao.
“Wanafanya vurugu Arusha ili watalii wagome kwenda huko, wanataka
watalii wakimbilie Kilimanjaro. Jamani tusiwakubalie hawa jamaa
wataliingiza taifa letu kubaya,” alisema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji
alisema kinachofanywa na CHADEMA mkoani Arusha na kwingineko kinaathiri
uwekezaji kwani wawekezaji watakimbilia nchi jirani.
Nagu alisema kutokuwapo kwa wabunge wa CHADEMA kumelifanya Bunge liwe tulivu tofauti na linavyokuwa wakiwapo wabunge hao.
Katika kile kinachoonekana wabunge wa CCM walijipanga kikamilifu
kukisulubu CHADEMA, kilichokosa wawakilishi, Waziri asiye na wizara
maalumu, Mark Mwandosya, alitumia kauli mbalimbali za mafumbo kukinanga
chama hicho cha upinzani.
Mwandosya alisema anaamini uchaguzi mkuu ujao, watu watachagua amani
dhidi ya vurugu, upendo dhidi ya chuki, amani dhidi ya vita huku kwenye
siasa watachagua vyama vinavyowaelekeza katika maendeleo na si vile
vinavyowaelekeza katika vurugu, migogoro na machafuko.
Kutokuwepo kwa wabunge wa CHADEMA pia kumeonekana kunatoa nafuu ya
mijadala ambapo Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema mijadala
mbalimbali iliyofanyika kwa siku nne imekwenda vizuri na Bunge limekuwa
kama la zamani.
Wakati hali ya mambo ikiwa si shwari ndani ya CCM, Kamishna wa
Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, juzi aliwaambia
waandishi wa habari kuwa wanawasiliana na makachero wao kuangalia hatua
za kisheria wanazoweza kuwachukulia viongozi wa CHADEMA waliogoma kutoa
ushahidi.
Alisema maelezo ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa waandishi
wa habari aliozungumza nao hivi karibuni ni tofauti na yale waliyoyatoa
polisi, hivyo jeshi hilo litaangalia
chanzo:daima