Msanii wa muziki wa kizazi kipya,marehemu Albert Mangwea enzi za uhai wake Dar es Salaam,Tanzania
WAKATI watu balimbali maarufu nchini, hususan wasanii wa muziki wa
kizazi kipya (Bongo Fleva), wakiendelea kutoa historia ya mahusiano yao
na aliyekuwa msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Albert Mangwea, msanii
maarufu wa muziki nchini Nassib Abdul (Diamond Platnumz) amevunja ukimya
na kutoa siri yake na marehemu Mangwea.
Akielezea hisia zake pamoja na mipango mingi aliyokuwa nayo kuhusu
kufanya kazi ya muziki na marehemu katika ukurasa wake wa mtandao wa
Instagram, Diamond alisema kwamba alijaribu kufanya kazi ya pamoja na
msanii huyo lakini kwa bahati mbaya kazi zote zikaharibika.
"Kinacho niumiza ni jinsi tulivyo jaribu kutengeneza HIT bila mafanikio
yaani siyo nilizo mshirikisha hata zile alizo nishirikisha na tuka amua
kuplan kutengeneza nyingine akirudi kutoka Afrika Kusini, lakini
haikuwezekana yani mungu alimpenda zaidi":alisema Platnumz.
Kila binadamu huwa na jambo lake muhimu ama siri ya mafanikio baina yake
na mtu mwingine ambayo pengine si rahisi kuizungumzia hadharani ama
wakati wowote, lakini inapotokea mmoja kati yao akifariki dunia
anayebaki duniani hujikuta akitoa siri hiyo.
Hatua ya Binadamu kuamua kutoa siri yake na mwenzake wakati wa msiba wa
mmoja wao inaweza ikawa na tafsiri nyingi lakini ukweli nikwamba huzuni
na machungu ya kuondokewa na mtu muhimu kwake aliyekuwa akitarajia
kufanya naye jambo flani muhimu ndiyo husababisha mtu huyo kutoa
siri.R.I.P Magwea.