Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, June 6, 2013

China yalinda haki na maslahi halali ya raia wake wanaoshikiliwa Ghana


China imeitaka Ghana ichukue hatua za kulinda usalama, haki na maslahi ya wachina wanaoshikiliwa nchini humo. Hayo yamesemwa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hong Lei, baada ya wachina 124 kukamatwa nchini Ghana katika zoezi linalofanywa na serikali ya nchi hiyo la kupambana na uchimbaji haramu wa madini ya dhahabu.

"wanadiplomasia wetu nchini Ghana wamewasiliana na maofisa wa ikulu ya Ghana. Tunaitaka serikali ya Ghana ifuate utaratibu wa kisheria katika zoezi hilo, kuzuia uporaji, kulinda usalama wa wachina na kuepusha haki na maslahi yao halali yasivamiwe."

Msemaji huyo ameongeza kuwa, bado hakuna ripoti kuhusu vifo au majeruhi ya wachina hao.

Mwandishi wetu wa habari aliyeko nchini Ghana ametoa ripoti kuwa, matumizi ya nguvu na matukio mengi ya uhalifu yametokea katika siku mbili zilizopita tangu serikali ya Ghana ianze kufanya zoezi hilo dhidi ya raia wake na wa nchi za nje wanaofanya uchimbaji haramu nchini humo, pamoja na wale waliouza leseni za uchimbaji na ardhi kwa watu wa nchi za nje.

Wachina wapatao 124 walikamatwa na polisi ya Ghana, ambao hivi sasa wanashikiliwa mjini Accra, wakisubiri kurudishwa nyumbani.

Mchina mmoja Bw Zhuo Yongxing aliyeshuhudia matukio hayo alisema, "polisi wa Ghana walikuja mgodini, wakapora kila kitu, halafu walichoma moto nyumba na mitambo yote, na kutunyang'anya pasipoti, simu za mkononi na pesa zetu zote. Tena waliwafyatulia risasi wachimbaji waliojificha mlimani kwa bunduki aina ya AK47."

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Ghana, zoezi hilo litadumu kwa wiki mbili.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...