Waziri Mkuu,Mizengo Pinda
Dodoma. Chama cha Maendeleo, Chadema kimeibuka jana bungeni na kusema
Serikali inafahamu ukweli wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa
chama hicho jijini Arusha.
Chama hicho kimesema Serikali ilitumia kutokuwepo kwao bungeni kupotosha
wananchi kuhusu hali halisi juu ya mlipuko wa bomu hilo uliotokea
wakati chama hicho kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa
udiwani katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha, Juni 15, mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kuanza kuchangia muswada wa sheria ya fedha ya
mwaka 2013/2014, Waziri kivuli wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
wa Chadema, Halima Mdee alisema, “Kabla sijaanza kuchangia Mheshimiwa
Spika naomba nianze kwa kuwapa pole wakazi wote wa Arusha kutokana na
mlipuko wa bomu uliosababisha watu kupoteza maisha, kwani tangu
limetokea tukio hilo leo ndiyo nazungumza kwa mara ya kwanza,”
“Tunazilaani kauli potofu zilizotolewa na Serikali hapa bungeni,
Serikali inajua nini kilichotokea Arusha na ilitumia kutokuwepo kwetu
kupotosha,” alisema.
CREDIT-MWANANCHI.COM
CREDIT-MWANANCHI.COM



