Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, June 6, 2013

BINTI WA MICHAEL JACKSON ANUSURIKA KATIKA JARIBIO LA KUJIUA

                                      Paris Michael Jackson anayesemekana alitaka kujiua.
PARIS, binti wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa Marekani, hayati  Michael Jackson, amelazwa hospitali baada ya kunusurika kujiua ikiwa ni siku chake kabla ya kutimia miaka minne ya kifo cha baba yake. Binti huyo ana umri wa miaka 15.
Binti huyo aliyelazwa hospitalini mjini Los Angeles anasemekana alimeza madawa kuliko kiwango kinachotakiwa.
Kwa mujibu wa Perry Sanders ambaye ni mwanasheria wa mama yake hayati Michael (Katherine Jackson), msichana huyo alichukuliwa na gari la wagonjwa saa 7.27 usiku na kupelekwa hospitali ambako hali yake inaendelea vyema.
Mwanasheria huyo pia hakutaka kuelezea sababu iliyomfikisha msichana huyo hospitali isipokuwa aliishia kusema tu kwamba hali yake inaendelea vizuri.
                                                           (Chanzo: The Independent)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...