Katika kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, mtangazaji huyo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika katika jamii.
Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu katika harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake.
Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale watazamaji katika tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee katika uga wa muziki.
Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee.
Credit: Mbondelewis Blog