Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Sunday, June 9, 2013

ALICHOKISEMA SAMWEL SITTA KUHUSU RASIMU YA KATIBA

Waziri wa  ushirikiano waAfrika Mashariki  Mh. Samweli Sitta amesema mchakato wa rasimu ya katiba mpya iliyotangazwa imelenga kuwatafutia  ulaji viongozi wa serikali na kwamba inahitajika kufanyiwa kazi  ya ziada na kudai kuwa muungano au shirikisho haviwezi kupatikana kama vipengele vinavyohusu serikali ya tanzania bara havijaelezwa vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kwenye mahafali ya chuo cha Ualimu Kibamba Mh Sitta amesema endapo kutakuwepo na rais wa tanganyika  ina maana nchi itakuwa kihoja kwa kuwa na marais watatu na kueleza kuwa kama yakipitishwa basi wananchi wakubali kuwepo na mzigo wa kuwahudumia na hata itifaki yake itakuwa ni tabu na kudai kuwa rasimu hiyo ni dhahiri viongozi wanajitafutia  ulaji ndani ya katiba mpya kwani haelewi ni kwanini tume imependekeza mawaziri  15 wakati masuala ya muungano yapo saba
 kwenye mahafali ya chuo cha Ualimu Kibamba Mh Sitta amesema endapo kutakuwepo na rais wa tanganyika ina maana nchi itakuwa kihoja kwa kuwa na marais watatu na kueleza kuwa kama yakipitishwa basi wananchi wakubali 
kuwepo na mzigo wa kuwahudumia na hata itifaki yake itakuwa ni tabu na kudai kuwa rasimu hiyo ni dhahiri viongozi wanajitafutia ulaji ndani ya katiba mpya kwani haelewi ni kwanini tume imependekeza mawaziri 15 wakati masuala ya muungano yapo saba

Credit: audifacejackson.blogspot.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...